Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Mark Simmonds, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza leo tarehe 11 Juni 2014. Pamoja na mambo mengine, Mawaziri hao wamezungumzia maazimio ya Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro (“End Sexual Violence in Conflict”) unaoendelea mjini London, Uingereza. Tanzania inashiriki mkutano huo kufuatia mualiko wa Serikali ya Uingereza kutokana na mchango mkubwa wa Tanzania katika kufanikisha kuwepo kwa Tamko la Umoja wa Mataifa linalohusu suala hilo (Declaration of Commitment to End Sexual Violence in Conflict).
No comments:
Post a Comment