MBUNGE wa Ileje, Aliko Kibona (CCM) ameomba Serikali ieleze juu ya ndege kutoka Malawi, ambayo imekuwa ikitia hofu wananchi wa Ileje, kwa kuzunguka angani kila mara.
Mbunge
huyo alisimama kutoa hoja hiyo baada ya kipindi cha maswali na majibu
na kuomba mwongozo wa Spika, Anne Makinda kuhusu suala hilo. Kibona
alisema:
“Nazungumzia
jambo mahsusi linalotokea katika mpaka wa Tanzania na Malawi katika
Jimbo la Ileje. Kwa sasa kuna ndege kutoka nchi ya Malawi inazunguka
katika vijiji jirani na tayari imeleta hofu kwa wananchi; na watoto
hawawezi kusoma. Ninaomba mwongozo wako kama nipo sahihi.
"Naitaka Serikali kwanza ieleze ile ndege inatoka wapi na inafanya nini; na Pili naitaka Serikali imfahamishe Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhusu ndege hiyo ili naye awafahamishe wananchi ili wasiwe na hofu”.
"Naitaka Serikali kwanza ieleze ile ndege inatoka wapi na inafanya nini; na Pili naitaka Serikali imfahamishe Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhusu ndege hiyo ili naye awafahamishe wananchi ili wasiwe na hofu”.
Kauli ya mbunge huyo imekuja wakati msimamo rais wa Malawi,
Profesa Peter Mutharika kuhusu mzozo uliopo kati ya nchi hiyo na
Tanzania kuhusu Ziwa Nyasa ukiwekwa bayana hatakuwa na mjadala kuhusu
mpaka wa nchi hizo akidai kuwa Ziwa Nyasa ni la Malawi pekee.
Kibona alisema kwa takriban wiki mbili sasa, ndege
hizo zimekuwa zikionekana upande wa Tanzania, lakini hakuna kauli
yoyote iliyotolewa na Serikali mpaka sasa.
Katika mwongozo wake, Spika Anne Makinda alisema:
“Jambo hili ni umuhimu sana hivyo Serikali ni lazima Serikali ijipange
ili kulijibu.” Aidha, Naibu Spika Job Ndugai aliongeza: “Hili jambo ni
zito na Serikali haiwezi kukurupuka kujibu. Kwanza lazima majibu hayo
yamfikie Rais Jakaya Kikwete.”
Profesa Mutharika, ambaye ni kiongozi wa Chama cha
Democratic Progressive (DPP), anapinga kuendelea kujadiliana na
Tanzania kuhusu nani mwenye haki ya kumiliki Ziwa Nyasa, msimamo aliutoa
kwa wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya
uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.
“Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana. Ziwa Malawi
ni mali ya Malawi na litaendelea kuwa la Malawi daima,” aliwaambia
wananchi hao huku akimshutumu mtangulizi wake, Joyce Banda kwamba
alikuwa dhaifu kiasi cha kutoa fursa kwa Tanzania kutumia udhaifu huo
kutaka kupora ziwa hilo.
Hata hivyo, akizungumza bungeni wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara yake, waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Tanzania ilikuwa
ikifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Malawi na kwamba iko tayari kufanya
kazi na serikali yoyote itakayoingia madarakani.
Juhudi za usuluhishi wa mzozo huo zinafanyika
chini ya uongozi wa rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chisano akisaidiwa
na rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki
No comments:
Post a Comment