Sepp Blatter |
Maafisa wa kandanda wa
Europa sasa wamemtaka rais wa shirikisho la kimataifa la kandanda FIFA, Sepp
Blatter, ajuzulu kutokana na madai ya rushwa yanayoindama Fifa.Wametilia shaka
uongozi wake.
Mkuu wa chama cha
soka cha uholanzi Michael Van Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter, Fifa
imeandamwa na tuhuma za rushwa na ili Fifa ijisafishe ni sharti Blatter ang’atuke.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa chama cha soka Uingereza , Greg Dyke, amesthtumu kauli ya Blatter
kuwa madai ya rushwa kuhusiana na kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe
la dunia 2022 yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na
ubaguzi wa rangi.
Blatter
anatarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania nafasi kipindi cha tano kuingoza Fifa
katika uchaguzi wa Fifa unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Kwa sasa wajumbe
wa Fifa wanavikao huko Sao Paulo wakijiandaa kwa ufunguzi wa kombe la dunia
hapo kesho ambako Sepp Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya
wale wanaoisema vibaya Fifa na Qatar.
No comments:
Post a Comment