Advertisements

Wednesday, July 23, 2014

MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA AUNGANA NA WAWAKILISHI WENGINE KUWAKUMBUKA WAHANGA WA MH17

Mhe. Balozi  Tuvako Manongi,  Muwakilishi wa  Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  jana  Jumatano ameungana na  Mabalozi   wengine wanaoziwakilishi    Nchi zao katika Umoja wa Mataifa,   kutia saini kitabu cha  maombolezo  kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa  Kudumu wa  Udachi ( Netherlandes) katika Umoja wa  Mataifa   kuwakumbuka watu 298 waliopoteza maisha baada  ya ndege waliyokuwa wakisafiria ya MH17 inayomilikiwa la  Shirika  la  Ndege la Malaysia  kuangushwa katika eneo la Mashariki ya  Ukraine wiki iliyopita. Idadi kubwa ya abiria hao walikuwa ni raia wa   Udachi.
 Balozi Tuvako  Manongi,akiandika katika kitabu  cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa  Udachi ( Nertherlands) kuomboleza familia 298   ambazo maisha yao yamekatishwa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria MH17 kuangushwa nchini Ukraine wiki iliyopita.
 Balozi akiwaombea marehemu
 Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, akizungumza machache na  Muwakilishi wa Kudumu wa   Udachi katika Umoja wa Mataifa,  Balozi  Karel van Oosterom mara baada ya Balozi Manongi  kusaini kitabu cha maombolezo.
"Asante sana kwa kuja  kutufariji katika kipindi hiki kigumu, asante sana, natambua vema ushirikiano  mzuri uliopo baina ya  serikali zetu".  ndivyo aliyosikika akisema  Muwakilishi wa Kudumu wa Udachi Balozi  Karel van Oosterom

No comments: