ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 13, 2014

NI UJERUMANI NA AJENTINA LEO

Leo ni fainali ya kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Ajentina na mpambano wa leo utafanya timu hizi kukutana fanaili ya kombe la Dunia mara tatu ambapo mara ya kwanza timu hizi zilikutana kwenye fainali ya kombe la Dunia mwaka 1986 wakati fanaili hizi zilipofanyikia nchini Mexico na Ajentina kuibuka mshindi kwa kuifunga Ujerumani kwa bao 3-2.

Mechi ya pili ya kukutanisha timu hizi katika fainali za kombe la Dunia ilifanyika mwaka 1990 nchini Italia na Ujerumani ikambanjua Ajentina kwa bao 1-0.

Mara ya tatu ni leo mwaka 2014 fainali zinazofanyika nchini Brazil na timu yeyote inaweza kuibuka na ushindi. Ukizingalia timu zote kwa haraka haraka utaona kitu kimoja kwama kila timu inacheza kitimu na kwa kufuata mafundisho ya walimu wao utofauti unakuja kwa kuanza na timu ya Ajentina ambao wao wapo imara kwenye ukuta zaidi na viungo na katika ufungaji wanategemea mchezaji mmoja au wawili  ambayo ni tofauti ni timu ya Ujerumani ambayo hujui umkabe nani mbele kila mchezaji anauwezo mkubwa wa kupachika mabao na timu inapokuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mara nyingi huibuka mshindi je kwenye ukuta wa Ajentina Wajerumani watafurukuta leo? ndio swali watakaojiuliza wengi lakini msema ukweli ni dakika 90.

No comments: