ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 10, 2014

WATU 6 WAMEUWAWA NA BAADAE MUUAJI AJISALIMISHA KWA POLISI.

PHOTO: Law enforcement officers investigate the scene of a shooting Wednesday, July 9, 2014, in Spring, Texas.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
PHOTO: A shooting suspect raises his hands as law enforcement officers surround him following a three-hour standoff, July 9, 2014, in Spring, Texas.
Muuwaji akinyoosha mikono juu kujisalimisha kwa polisi

Jamaa mmoja mkazi wa Texas alienda kwenye nyumba ambayo ndugu zake walikuwa wakiishi kwenye mji wa Spring, Texas nchini Marekani siku ya Jumatano na kufyatua risasi na kuua watu 6 wa familia moja wakiwemo watoto wa wanne wenye umri wa miaka 4, 13 na baadae akajisalimisha polisi. Muuaji Ron Haskell, 34 anayeshikiliwa polisi atafikishwa mahamani na kushitakiwa kwa mauwaji hayo.

Binti wa miaka 15 pekee aliyenusurika katika mauaji hayo ndiye aliyetoa taarifa polisi kwa kupiga simu 911 na kuwataarifu polisi kuwa mtu ameingia nyumbani wao na kuwaua ndugu zake sasa hivi binti huyo yupo mahututi hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya na risasi  za muuwaji huyo.

Waliouwawa ni watoto wakiume miaka 4-13 na watoto wa kike miaka 7-9 wakiwemo baba wa miaka 39 na mama wa miaka 33 waloikutwa wamekufa eneo la tukio.

Muuwaji alikua amevaa nguo za kampuni ya FEDEX na alijaribu kukimbia lakini hakufika mbali baada ya kujikuta amezingirwa na polisi kila upande na baadae aliamua kujisalimisha.

1 comment:

Anonymous said...

Kwakweli inasikitisha sana. Hii yote ni kwasababu alikuwa anamtafuta ex wife wake sasa alitegemea angemkuta nyumbani kwa dada yake.( aliyeuawa ni ex sister inlaw mumewe na wanae wanne. Na alikuwa anaelekea nyumbani kwa his ex inlaws kuwaua pia. Ila alikamtwa kabla ya kufika. Thanks to the 15yrs old girl who acted like she was dead and called 911. May their gentle and loving souls rest in peace. And may God almighty give the beautiful 15 yrs old courage and strength to overcome such a tragic loss.