ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 11, 2014

Zanzibar Beach Soccer Bonanza kumekucha

Na Andrew Chale
TAASISI ya Mwangaza wa buradani Zanzibar (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja, Zanzibar, kupitia vyombo vya habari, imemtangaza rasmi , Raisi mstaafu wa Chama cha Soka Zanzibar, (Zanzibar Football Association-ZFA) Mzee Ally Fereji Tamim kuwa mgeni rasmi kwenye michuano maalum ya soka la ufukweni lijulikanayo kama (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti Mbili mwaka huu katika fukwe za Nungwi.
Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa, michuano hiyo ya Zanzibar Beach Soccer inatarajiwa kuzikutanisha timu mbalimbali za Visiwani humo, Bara na nje ya Tanzania ambapo watakutana kwa pamoja na kushiriki kichuano hiyo maalum, kwenye fukwe hizo za Nungwi.
Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema wamejisikia furaha kwa viongozi wa juu na wadau wa soka kuwaunga mkono, kwani inatia moyo katika kuendesha shughuli za kimichezo kama hizo. “Tunapongeza wadau wote, kikubwa zaidi, ni Mzee wetu, Ally Fereji Tamim kukubari kuwa mgeni rasmi, pia milango ipo wazi kwa wadau wengine kujitokeza katika kufanikisha zaidi tukio hili ,muhimu” alisema Muslim Nassoro ‘Jazzphaa’.
Aidha, aliendelea kuwaomba mashirika, makampuni, taasisi za Serikali na za watu binafsi na wadau kujitokeza kwa wingi kudhamini Bonanza hilo la Zanzibaar Beach Soccer, ilikufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuifikia jamii na kuiweka pamoja.
Muslim Nassoro ‘Jazzphaa’ aliongeza kuwa, Michezo hiyo yenye lengo ya kuweka watu pamoja, kudumisha utamaduni na kuhimalisha afya ya mwili, pia itakuwa na burudani mbalimbali. Lakini pia alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa beach soccer na kamati yote kwa ujumla katika kufanikisha jambo hilo.
Kwa upande wake, Rais wa beach Soccer Zanzibar, Bwana Ally Sheikh Alhabshy alipongeza Taasisi hiyo kuandaa michuano hiyo ambapo amesisitiza kuwa Wadhamini wasisitite kutoa udhamini wao na kuja kuona mchezo huo unavyochezwa.
Zanzibar Beach soccer Bonanza kwa mwaka huu itakuwa ni ya mara ya tatu, kwa taasisi hiyo kuandaa michezo hiyo ya soka la ufukweni.
Michezo hiyo ya soka la ufukweni imekuwa maalufu katika nchi mbalimbali zenye fukwe, ambapo wananchi na wageni kutoka mataifa mengine ujumuika kwa pamoja.
Kwa mwaka huu pia kutakuwa na burudani kali na ya aina yake itayaoporomoshwa na dj mkali anayetikisa visiwani humo.

No comments: