Monday, August 11, 2014

ALICHOKIFANYA FLAVIANA MATATA FOUNDATION

Flaviana Matata foundation ambayo imeanzishwa na model Flaviana Matata siku ya leo (11/8/2014) itakuwa mkoani Lindi katika muendelezo wa kazi za kuchangia elimu.

Timu ya FMF itakuwa kwenye shule za msingi Mtua huko Nachingwea na Litingi iliyopo Lindi Mjini. Wanafunzi 700 wa shule hizi mbili watapokea vifaa vya shule kutoka Flaviana Matata foundation ambapo shughuli hii imedhaminiwa na PSPF.

Flaviana Matata foundation imewai kufanya kazi kama hizi sehemu tofauti kama Bagamoyo na sehemu nyingine kwenye project za FMF back to school project.
Credit:Millard Ayo.com

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake