Friday, August 15, 2014

BABU TALE AZUNGUMZIA BEEF LA DIAMOND NA ALI KIBA

Meneja wa Diamond, Babu Tale amezungumzia kile kile kinachoelezwa kuwa ni beef kali ama ushindani mkubwa kati ya Diamond na Ali Kiba, moja kati ya mada ambazo zinatengeneza mijadal mingi sana kwenye mitandao ya kijamii,

Akizungumza kupitia kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm, Babu Tale amejibu swali la msikilizaji aliyetaka kufahamu mtazamo wake kuhusu uwepo wa beef kati ya wasanii hao wawili. 

“Mimi sidhani kama Diamond na Ali Kiba wana beef, ni biashara…challenging. Sijawahi kuona wanagombana katika maisha yangu. Watu wanaoandika nyuma wanaandika kwa sababu wanaamua kuandika lakini mwisho wa siku Diamond na Ali Kiba wote ni wanamuziki. Without challenge Diamond hawezi kuendelea au Ali Kiba hawezi kuendelea.” Amesema Babu Tale. 


Ameeleza kuwa hiyo kwake anaona challenge hiyo ni nzuri kibiashara na sio tatizo na kwamba likionekana ni tatizo watalitatua. 


“Kama unamfollow Davido na Wizkid. Kila anapopost Wizkid kwamba hapa nafanya show hivi, Davido nae anamjibu kuwa angalia watu wamejaa huku hivi. Ni biashara. Ugomvi wanagombania nini? Ali Kiba anakula kwale ana maisha yake, Diamond anakula kwake na ana maisha yake.” Ameongeza Babu Tale. 


Alipoulizwa kuhusu ujio wa Ali Kiba kuchukuliwa kama ndio sehemu ya mapinduzi dhidi ya utawala wa Diamond, Babu Tale aliipinga kauli hiyo. 


“Huwezi kusema Ali Kiba anakuja, Ali Kiba yupo na alikuwepo. Huwezi kumuambia anakuja unamdhalilisha, Ali Kiba yupo alikuwepo na ana uwezo wake. Anafahamu base yake. Huwezi kumwambia anakuja, anakuja ni msanii mpya…Raymond wa Tip Top anakuja sio Ali Kiba. Usiwe na mind kuwa Ali Kiba hayupo kwenye Game, yupo.” 


Ameongeza kuwa hajafirikia kuhusu suala la Ali Kiba kumpindua Diamond.
Credit:Pro24

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake