Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Titus Naikuni anasisitiza kuwa licha ya shirika la afya duniani WHO kuiweka Kenya miongoni mwa mataifa yaliyo hatarini kuambukizwahoma ya ebola kutokana na kuwepo kwake kama kitovu cha mawasiliano barani Afrika , WHO haijawathibitishia kuwa kuna uwezekana wa kuambukizwa Ebola mjini Nairobi.
Naikuni aliendelea kusema kuwa mashirika mengi ya ndege yanaendelea kuhudumu katika ukanda huo wa Afrika Magharibi.
Hapo Jana Muungano wa Madakatari nchini Kenya Ulizua taharuki ulipotangaza kuwa haupo tayari kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa ebola mjini Nairobi Kenya kufuatia mgomo unaoendelea wa wauguzi na ukosefu wa fedha.
Aidha wabunge walitoa taarifa ya kuitaka shirika hilo la ndege kukomesha safari zake kuelekea magharibi mwa Afrika hadi pale ugonjwa huo utakapokuwa umethibitiwa kikamilifu.
Chama cha wahudumu wa afya nchini Kenya kiliitaka serikali ya Kenya kuishinikiza shirika hilo la ndege ilikuepuka kuenea kwa ugonjwa huo.
Chama hicho kilisema kuwa Kenya Airways linahatarisha zaidi maisha ya wakenya kwa kutoa huduma kwenda katika miji ambayo kwa sasa inatajwa kuwa na ugonjwa wa ebola.
Mwenyeki wa chama hicho Daktari Elly Opot alisema kuwa Kenya haijajianda kikamilifu kuweza kukabiliana na ugonjwa wa ebola ikiwa itabainika kuwa ugonjwa huo umefika nchini Kenya.
Licha ya kuwa mashirika tofauti ya ndege yamefutilia mbali safari zao kuelekea Magharibi mwa Afrika Kenya Airways imesema kuwa itaendelea kuwasafirisha abiria licha ya milipuko ya Ebola.
Kenya Airways inasema imechukua hatua hiyo kufuatia tangazo la shirika la Afya Duniani, WHO, kuwa uwezekano wa abiria kuambukizwa maradhi kwa kutembelea eneo hilo tu ni duni sana.
Kenya Airways inasisitiza itaendelea na safari kuelekea maeneo yenye Ebola licha ya shinikizo la wadau nchini Kenya.
Kenya Airways inasema kuwa imewahamasisha wafanyakazi wake wote kuhusiana na jinsi maradhi hayo ya Ebola yanavyoambukizwa na kuwa wamepewa vifaa vya kinga.
Wizara ya Afya ya Kenya ilitangaza juma lililopita kuwa haitaunga mkono mapendekezo ya kuweka vikwazo vya kibiashara au usafiri kwa eneo linalotajwa kuwa na virusi vya maradhi hayo.
Watu wote walioambukizwa virusi vya Ebola nchini Nigeria wamethibitishwa kuwa waligusana na mtu aliyetua Lagos kutoka Monrovia na baadaye akafariki.
Shirika la ndege la Uingereza, British Airways, baadhi ya mashirika mengi yamesitisha ndege zake kwenda Lagos na Monrovia hadi mwisho wa Agosti.
Zaidi ya watu 1000 wameaga dunia nchini Sierra Leone, Liberia, Guinea na Nigeria katika kile kinachotajwa kuwa mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa wa Ebola kuwai kushudiwa.
BBC
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake