Friday, August 15, 2014

Itachukua miezi sita kudhibiti Ebola

Mkuu wa shirika la madaktari wasio na mipaka la Medicins Sans Frontieres, amesema kuwa itachukua miezi sita kuweza kudhibiti janga la Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Akizungumza mjini Geneva,mkuu huyo, Joanne Lui alisema kuwa uongozi mzuri unahitajika kutoka kwa shirika la afya duniani na kwamba kukabiliana na Ebola hasa ilikozuka mwanzo nchini liberia, ni muhimu zaidi katika kumaliza ugonjwa huo.

Hasa amesisitiza kwamba wataalamu zaidi wenye uzoefu wa kupambana na ugonjwa hupo wanahitajika katika maeneo yaliyoathirika.

Bi Lui aliongeza matabibu 80 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, huku watu wengine 170 wakiambakizwa na kwamba nyingi ya vituo vya afya vimefurika wagonjwa wa Ebola.

''Ikiwa hatutapambana na ugonjwa huo nchini Liberia,basi itakuwa vigumu kuudhibiti katika kanda nzima ya Afrika Magharbi,'' alisema Bi Lui.

Mifumo ya afya katika neo la Afrika Magharibi inakabiliwa na hali ngumu wakati huu wa mlipuko wa Ebola.

Ebola huambukizana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, kupitia maji maji ya mwili au damu.

Dalili kama za mafua zinaweza kusababisha mtu kuvuja damu kutoka kwenye sehemu zake za mwili kama vile masikioni, mapuani, machoni na ndani ya mwili na kusababisha viungo vya mwili kutofanya kazi.

BBC

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake