Mwanamuziki wa Bongo Flavor Nchini Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinums, amesema hajaridhika na malipo sasa kimuziki, ndio maana kila siku anajifunza kwa kufuatilia kwa ukaribu maisha ya Nyota wengi hasa wanamichezo Kutoka Mataifa Tofauti Duniani.
Diamond ambae ni miongoni mwa wanamuziki waliofanya vyema kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta Mkoani Mwanza hivi karibuni, ametoa taarifa za kuwafuatilia nyota hao mbalimbali kwenye mahojiano maalum na Shaffih Dauda, kupitia Dauda TV.
Miongoni mwa nyota ambao Diamond anawafuatilia hasa kupitia Mtandao wa Instagram, ni Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon Samuel Etoo, Kiungo Mshambuliaji wa Brazil na Barcelona Neymar, Bondia Mmarekani Floyd Myweather na wengineo.
Pamoja na Diamond kuweka hilo wazi, pia amesema aliwahi kucheza masumbwi, kisha akahamia kwenye Soka hasa nafasi ya golikipa na namba sita yaani kiungo Mkabaji, lakini aliamua kuachana na Soka baada ya mama yake kumsihi kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Awali kulikuwa na hisia kwamba Diamond anashabikia timu ya Dar-es-salaam Young Africans, hasa baada ya kuweka picha kwenye mitandao akiwa na Mrisho Ngasa mara kadhaa, lakini amesema yeye na Ngasa ni marafiki, na sio mshabiki wa Yanga kama inavyodhaniwa.
Diamond ameongeza kwa kusema sio tu haishabikii Yanga, bali kwa hapa nyumbani hana timu anayoishabikia, badala yake anaipenda FC Barcelona ya Hispania, ambapo amesema kuna kipindi mapenzi yalizidi kwa timu hiyo, kiasi cha kuweza kupanga kikosi chote.
Credit:Shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake