Wednesday, August 13, 2014

MAMA TUNU PINDA ATUNUKIWA CHETI CHA UBALOZI WA AMANI DUNIANI

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa UPF, Dk. Charles Yang mara baada ya kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na viongozi wenzake 10 waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na viongozi wengine waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini. Walioshika vyeti kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa visiwa vya Samoa, Bibi Filifilia Tamasese , Mke wa Rais wa visiwa vya Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak na Mke wa Rais wa Fiji, Bibi Koila Nailatikau. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake