Advertisements

Monday, August 18, 2014

MAULID KITENGE ATUA RADIO EFM RASMI

Mtangazaji mahiri wa habari za michezo, Maulidi Baraka Kitenge akisaini mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM, Dickson Ponela.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo, Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM, Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya radio hiyo, yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

MTANGAZAJI mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar es salaam leo.

Kutokana na tafiti ya Ipsos ya mwaka 2013, inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Radio One, ndiye mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM, Dickson Ponela, ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Kitenge ameisha saini mkataba na kituo chetu na anatarajiwa kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji waliobobea katika fani hiyo akiwemo Dizo One, Dennis Sebo, Sos B, Kanky Mwaigomole na Dj Majay.
Credit:GPL

No comments: