Saturday, August 16, 2014

MAZISHI YA SAIDI "CHOCOLATE" COPENHAGEN, DENMARK LEO JUMAMOSI


Said :Chocolate" enzi ya uhai wake,
Watanzania nchini Denmark na nchi jirani wakijumuika pamoja kwenye mazishi ya Marehemu Said Chocolate aliyezikwa leo Jumamosi Aug 16, 2014 mjini Copenhagen, nchini Denmark. Marehemu Said alikutwa na mauti siku kadhaa nyumbani na kugunduliwa amekufa na rafiki yake wa karibu na ni baada ya kujaribu kumpigia simu kwa siku kadhaa bila majibu na hatimae kuamua kufika nyumbani kwake na alipochungulia kwenye mlango na kukutana na harufu kali ndipo aliporipoti polisi na polisi kufika na kuvunja mlango na kukuta mwili wa marehemu umeishaanza kuharibika. Marehemu ameacha mtoto aliyekua amezaa na matalaka wake wake miaka ya nyuma ambaye ni raia wa Denmark. Mungu ilaze roho ya marehemu pema peponi, Amina.
Mazishi ya marehemu Said Chocolate yakiendelea na kujuisha Watanzania wa Denmark na marafiki zao.
Baadhi ya Watanzania waliojumika kwenye mazishi ya mwenzao wakiwa katika picha ya pamoja. 
 Watanzania wa Denmark na nchini jirani wakijumuika pamoja kwenye mazishi Mtanzania mwenzao marehemu Said aliyezikwa leo siku ya Jumamosi jijini Copenhagen, Denmark.
 Maziko yakiendelea.

4 comments:

  1. REST IN PEACE ! SAIDY UPO NASI BADO KIMAWAZO, JAPO HATU KUONI

    ReplyDelete
  2. Ila kiukweli watanzania tuishio nje tuna tisha hasa hapa Canada.hatunaga ile kujuliana khali sijui ndio ubusy wa kubeba box.maana nakumbuka kuna Dada moja aliumwa ndani wiki kadhaa bila watu wake wa jirani kujua Kama tungekuwa na ile khali ya kujiuliza Hivi huyu mtu hatujamuona siku mbili Tatu.tumjulie khali haya hayawezi kutokea.rest in peace.nampongeza huyo kaka aliyegundua

    ReplyDelete
  3. watanzania tuliopo ughaibuni tuwe na moyo wa kujuliana hali hapa tumekuja kutafuta ughaibuni tuwe kitu kimoja jamani please.tuache mapungufu yetu sisi ni binadamu na tushike kamba ya Allah amin.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake