ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 16, 2014

MKUTANO WA WANAJUMUIYA WA NEW YORK TANZANIA COMMUNITY (NYTC) LEO JUMAMOSI KUANZIA SAA KUMI JIONI HADI SAA MBILI USIKU.

TANGAZO LA MKUTANO WA JUMUIYA NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY:

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York (New York Tanzanian Community) una furaha kubwa kuwakumbusha na kuwakaribisha Watanzania wote walioko New York, New Jersey, Pennsylvania na Connecticut kwenye Mkutano wa Wanajumuiya ambao utaambatana na BBQ.

Lini : Jumamosi, tarehe 16 August 2014.

Muda: 4pm -8pm (Please plan to arrive on time. This event will end promptly at 8pm)

Wapi: Nyumba ya Ubalozi iliyopo 30 Overhill Road, Mount Vernon, NY 10552

Nia na madhumuni ya mkutano huu pamoja na BBQ ni kuwapa nafasi Wanajumuiya na Viongozi wa Jumuiya kujumuika pamoja katika kupeana mawaidha ya maendeleo ya kusogeza mbele jumuiya na pia kushereheka kabla ya kuisha kwa msimu wa Summer.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na viongozi wako wa Jumuiya kama ifutavyo:

Mwenyekiti: Hajji Khamis, Tel. 347-623-8965
Makamu Mwenyekiti: Michael Chiume, Tel. 646-662-6999
Katibu: Deogratius Mhella, Tel. 917-531-7546
Katibu Msaidizi: Miriam Abu, Tel. 914-316-2814
Mweka Hazina: Raphael Faida, Tel. 347-869-2230
Mweka Hazina Msaidizi: Dr. Anicetus Temba, Tel. 347-489-6532
Please feel free to support this event by bringing your favorite Tanzanian /non-Tanzanian dish, appetizers and drinks of all kinds including water.

Karibuni sana.
Hajji Khamis
Mwenyekiti, New York Tanzanian Community.
TO ALL MEMBERS: ASK WHAT YOU HAVE DONE FOR THE COMMUNITY AND NOT ASK WHAT THE COMMUNITY HAS DONE FOR YOU".
Huyu ni mtaalamu wa kuchoma nyama bwana Lucas.

22 comments:

Anonymous said...

wapi shabani mseba?mbona majina mapya

Anonymous said...

shabani mseba yuko bongo anakula ugari wa chenga

Anonymous said...

mnajua kilichomsibi shabani mseba msilete umbeya wenu acheni zenu bwana.

Anonymous said...

yaleo kali mmeamuwa kuweka hiyo picha ya shabani msebu haaaaa

Anonymous said...

mbona wanawake kwenye huu huongozi naona mmoja tu? ni umoja wa akina baba only?

Anonymous said...

Huyo wa nne aliyetoa komenti sio Miriam kweli?

Anonymous said...

kumbe sahabani anawakosesha usingizi eeeh...

na wewe mdau huyo wa nne ni "Anonymous" na siyo miriam. watu wengine bwana, mtu keshaamua kuwa anonymous watu mnataka kuchokonoa au hamjui maana ya anonymous?

Anonymous said...

mariam ndo nani tena?

Anonymous said...

Community yetu inahitaji viongozi wanawake miriam ndie pekeyake alio jitokeza kwenye uchaguzi kama wewe nimwana mke jingize kwenye uchaguzi kama hatukuchagua basi tuta kuteuala zima tupate mashujaa wakike kwenye uongozi

Anonymous said...

Please hakuna haja ya kujieleza mmoja mmoja kwani tunawalipa?.Hiki chama cha wote not me, myself and I. Chama ni wote si viongozi tu. We need to focus in what Chama is doing and will do.

Anonymous said...

Hongera Katibu Mhella. Kikao tumekuwa tukikisubiri kwa hamu. Tunakuunga mkono Katibu wetu.

Anonymous said...

Pole Katibu na majukumu. Tupo wote. Tutafika.

Anonymous said...

Na Mimi naunga mkono. Mhella tutakuja kwa wingi. Husikubali wavuruge kikao nasikia mizengwe mingi ... Gangamala Mhella, tulikuchagua ututetee

Anonymous said...

Tunashukuru safari hii sisi wa Mount Vernon mmetukumbuka. NYTC oyee!

Anonymous said...

afadhali nyie wa NYC mna umoja unaeleweka, sis huku DC ni majanga mie binafsi natamani kuhama

Anonymous said...

Mbona chama cha shari sana? Awatetee kwani katibu aliwaleta Mmarekani au anawaweka mjini?

Anonymous said...

HUYU ANAE POST HIZI COMMENT SIO DEOGRATIUS MWENYEWE LAKINI 1+1=2

Anonymous said...

Mdau wa tarehe 25 July saa 12:52 pm unaonyesha ni jinsi gani usivyo na mapenzi na Jumuiya hii. Na jinsi ulivyo
Mbinafsi.

Anonymous said...

Duh nilishakaa mkao wa kula nyama za mzee Lucas.

Anonymous said...

Sidhani kama hapendi chama nadhani ana maanisha hamna haja ya viongozi kujieleza wametufanyia nini mmoja mmoja. Sisi wanachama tunabidi tuje na mikakati tunataka kufanya nini ili chama kiendelee. We can't be too passive and wait for our leaders to be the remote controls. We need to be creative to produce ideas of how our community can thrive.

Anonymous said...

Wanajumuiya hatujafanya Kikao siku nyingi. Hiki Kikao ni muhimu.

Anonymous said...

Vizuri tutajumuika. Undugu hazina yetu.