Wiki ya jana tuliona namna Mpishi alivyo mtu muhimu katika
jamii kuliko wafanyakazi wote unaoweza kuwaajiri na hoja kuu ikiwa kwamba
Mpishi ndiye anayechanganya kemikali unazokula na kukufanya uwepo, tena katika
afya njema. Baunsa, Mwanasheria, Dereva, Mshauri, Daktari na hata Mwalimu na
wengineo wote hawana fursa ya kupata ajira kwako endapo mpishi hakutekeleza
majukumu yake ipasavyo ili wao wakuone. Unaweza ukamuajiri rasmi mpishi wako,
lakini hata kumwajiri kwa masaa ‘Part time’ pia inawezekana na akakupa ushauri
mzuri juu ya afya yako na vyakula.
Mpishi ana nafasi kubwa kuliko daktari katika tiba ya
ugonjwa wa kisukari, na dunia nzima inaelewa hivyo. Kisukari, yaani ‘Diabetes
Mellitus’ ni maradhi yatokanayo na sukari kuzidi katika mzunguko wa damu
mwilini. Hii hutokea iwapo kiungo kiitwacho kongosho hakitazalisha ‘insulin’ au
kitazalisha insulin kidogo kwa mahitaji ya sukari kugeuzwa kuwa nishati ‘Calories’
za kumwendesha binadamu. Dalili za maradhi haya huwa hazijifichi: Kiu ya
marakwa mara, njaa ya mara kwa mara, Uzito hupotea bila taarifa rasmi, macho
huanza kufa taratibu na maambukizi ya mara kwa mara pamoja na homa za kujirudia
rudia humkumba mgonjwa kwa kuwa kinga ya mwili nayo pia hushuka.
Wagonjwa wasiozalisha kabisa insulin hawa huitwa ‘Insulin
Dependant’ ambapo mara nyingi hujitokeza toka utotoni kwa kuwa na ulemavu wa
aina tofauti katika kongosho. Wagonjwa hawa huhitaji sindano moja au zaidi ya insulin ili kupata
mchanganyo sawa na kiwango cha sukari mwilini. ‘Non Insulin Dependant’ hawa ni
aina ya pili ya wagonjwa wa kisukari ambao kwa kawaida ni wengi sana na
huwatokea wakiwa watu wazima kabisa. Wao, kongosho huzalisha insulin kama
kawaida yake ila huwa haitoshelezi mahitaji ya sukari iliyopo mwilini kutokana
na sababu tofauti lakini kubwa ikiwa ni unene ambao ni tatizo kwa wengi, msongo
wa akili pia husababisha kisukari na hata wazazi wenye kisukari hurithisha
watoto kwa 50%.
Wanawake waliojazia mitaa ya shingo, kifua, mabega na tumbo
wapo hatarini au wameshaukwaa ugonjwa huu ukilinganisha na wale walijazia
sehemu za makalio na mapajani zaidi. Ila, tafiti za tiba zinatoa uhakika wa
tiba kwa lishe kupitia mpishi mbobevu ambaye huponyesha kabisa ugonjwa huu kwa
kumpa mgonjwa lishe maalum hasa wagonjwa wa ‘Non Insulin Dependant’ ambao
hupona kwa asilimia 58% wengi wao wakiwa ni wazee wa miaka 60 na kuendelea.
Mafanikio hupatikana baada ya mpishi kupa mgonjwa vyakula visivyo na kalori
nyingi huku akimhimiza mgonjwa kufanya mazoezi na hapo mgonjwa hupoteza 5%-7% ya
uzito wake kwa siku. Hii itamsaidia mgonjwa kupona kwa kuwa seli za misuli ya
mwili hupata nafasi ya kuidhibiti sukari kikamilifu zaidi.
Kwa kawaida, wagonjwa wa kisukari, wazee, na watu
wanene(Obese) huhitaji kiasi cha kalori 1000 hadi 1600 kwa siku nzima. Mpishi
atapunguza kiwango cha kalori 500 kati ya hizo na atafanikiwa kumpunguza uzito
mgonjwa kati ya kilo 2 hadi 4 na uhakika upo wazi kweupe. Hata hivyo, mgonjwa
atahisi mpishi amebadilisha mapishi kwani vinywaji baridi, vyakula vya mbegu,
vyakula vya kukaanga, mafuta, sukari na chumvi bila kusahau ‘chachandu’ yaani
achali hubeba kalori nyingi sana hivyo mpishi ataviondoa katika mlo wa mgonjwa.
Ila, kukosa mafuta, chumvi na sukari bado sio sababu ya msingi kwa mpishi
kukupa vyakula vyenye ladha kwani Mungu ameumba vyakula bila idadi duniani.
Wiki ijayo, tutaangalia pia ni namna gani mpishi anavyoweza
kupambana na homa hivyo usikose nakala yako ya UWAZI jumanne. Sote tumeona
namna mpishi alivyo bora kuliko mtu yeyote unayeweza kumwajiri. Ukiwa na swali,
hoja, maoni au ukahitaji ushauri wa kina basi tupigie na utembelee mtandao wetu
hapo juu.
Joh Haule
0768 215 956
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake