ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 13, 2014

MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI WAUNGUA

MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI WAUNGUA
Msikiti maarufu wa Mtambani uliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam waungua. Hadi muda wa saa moja na nusu usiku huu, magari ya zima moto yameonekana eneo la tukio yakijaribu kuuzima moto huo, ingawa kazi ya kuuzima imeonekana kuwa ngumu kutokana na moto kuanzia ghorofa ya juu ya msikiti huo. Magari ya zima moto yanaendelea kutafuta mbinu ya kufikisha mipira ya maji juu ya jengo hilo, ambalo chini huwa ni msikiti na juu ni madrasa. Hizi ni baadhi ya picha za tukio kama zilivyotumwa na mwandishi wa Global Publishers aliyeko eneo la tukio.

PICHA: SHAKOOR JONGO/GPL

No comments: