Thursday, August 14, 2014

MTOTO ANAEDAIWA KUFICHWA NA KUTESWA AZUNGUMUZA NA WAANDISHI WA HABARI

Mtoto Colins Silvanus Mzeru mkazi wa Tabata Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana alipofika na mamayake mlezi, Nora Mzeru kukanusha tuhuma dhid i ya mamayake huyo kuwa amemfungia na kumtesa kwa muda mrefu sasa na kushindwa kwenda shule.

Colins amesema mama yake huyo mlezi hana tatizo nae na amekuwa akiishi nae kwa muda mrefu sasa vizuri tangu kufariki kwa mama yake mzazi na yeye kuchukuliwa na baba yake na kupokelewa bna mama yake huyo aliyekuwa akiishi na baba yake na kulelewa vizuri hadi sasa licha ya kuwa baba yake mzazi nae kufariki.

Bi Nora Mzeru ambaye ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ilala amekanusha vikali taarifa zilizokuwa zikirushwa na Kituo kimoja cha Redio maarufu jijini Dar es Salaam juu ya kuteswa kwa mtoto huyo na kudai kuwa wanaofanya hivyo wanalenga kumchafua na ambapo amesema wanaofanya hivyo ni mama wadogo na wajomba wa Colins ambao wameanza kufanya hivyo tangu kufariki kwa mumewe.- Father Kidevu

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake