Friday, August 15, 2014

Mwanamuziki kamanda ras makunja afunguka kuhusu mabadiliko ya katiba na pia uraia pacha


KIONGOZI WA NGOMA AFRICA BAND KAMANDA RAS MAKUNJA AFUNGUKA !




KUHUSU HAKI YA URAIA NA URAIA PACHA ! 
SI SWALA LA WENGI WAPE BALI NI HAKI YA BINADAMU NA PIA URAIA!
WENGI WANAHITAJI KUELIMISHWA!

MTAZAMO WA KATIBA MPYA NA MTANZANIA KWANZA


Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mtunzi,mwimbaji kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma africa band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, amefunguka na machache yafuatayo kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania na haki za raia wa Tanzania:

Akizungumza kutoka katika makao yake mjini Oldenburg,Ujerumani.
Kamanda Ras Makunja wa kikosi kazi FFU-Ughaibuni alisema
Kuwa: MCHAKATO WA KATIBA MPYA UMEWAFANYA WATANZANIA
WENGI KUSOMA KATIBA YA ZAMANI ! MWANZO WALIKUWA HAWAISOMI NA KULIELWA VEMA ! 
Kwa sasa ! WATANZANIA HATUNA HAJA YA KUOGOPA  MAUMIVU YA 
MABADILIKO YA KATIBA LAZIMA TUENDE KUFUATANA NA WAKATI,
LAZIMA TUWEKE MASALAHI YA TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA,

Ras Makunja,alichambua zaidi kwa kusema kuwa watanzania tumekuwa tunatabia za uwoga wa maumivu ya mabadiliko linapokuja swala la kujadili masilahi ya kitaifa na mtanzania,mara nyingine bila ya kujijua tunawapigania
watu ambao sio walengwa katika katiba "Nina maana walengwa wa kunufahika katika katiba hii lazima wawe watanzania wote wa bara na visiwani ambao wanaishi popote pale duniani" bila kujali dini,jinsia au
vyama vyao vya kisiasa.

SWALI: NINI ? MTAZAMO WAKO NA UNATARAJIA NINI ? KATIKA KATIBA MPYA ?

RAS.MAKUNJA: Mtazamo wa wangu katika kulijadili hili la katiba mpya ningewaomba kwanza wale wabunge walio katika bunge maalumu la katiba
kwamba : WAFANYE KILA HALI KATIKA MJADALA HUU KUPATA KATIBA
YENYE MASILAHI 99% TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA

Mfano: Haki za kumiliki Ardhi,tunapoongelea swala la Haki ya mtanzania
basi Ardhi na maslahi yanayo patikana katika Ardhi lazima yamilikiwe na
raia wa Tanzania kwanza,kwa sababu Ardhi ndio msingi au ubongo wa nchi yetu,kwa maana hii asilimia kubwa ya ardhi kama haipo katika miliki ya raia
wa Tanzania ,uhuru wetu unatakuwa umepungua maana.
ARDHI NA RAIA WA TANZANIA NDIO MOYO WA TAIFA NA UTAWALA
WA TANZANIA,asilimia 50% ya Adhi ikiwa mikononi mwa watu ambao sio
watanzania,au watu ambao wana offer za kukaa au kufanya jambo katika
ardhi kwa mktaba wa miaka mingi ,wananchi tutajikuta tupo ugenini katika ardhi yetu.HII HAINA MAANA KUWA TUNAWAFUNGIA MILANGO WAWEKEZAJI BALI TUNAWEZA KUINGIA NAO MIKATABA YA MUDA MFUPI .

SWALI:  KUHUSU URAIA PACHA UNALIONAJE HILI?

RAS MAKUNJA: SIO SWALA LA WENGI WAPE ! NA WACHACHE WANYIME BALI SWALA LA HAKI YA BINADAMU NA URAIA

WATANZANIA LAZIMA TULITAZAME SWALA URAIA PACHA KWA FAIDA YA TANZANIA NA PIA TULICHAMBUE HASARA NA FAIDA ZAKE.
Ras Makunja aliingia kwa kina kwa kusema kuwa kuhusu uraia pacha
walio wengi wanahitaji kuelemishwa faida na hasara zake,pamoja na haki
za msingi kwa watanzania wanaomba hili liwemo katika katiba mpya.
Kwanza tunapolizungumzia hili lazima tujue nini ?maana uraia na nini maana Pasipoti.
Historia inaonyesha kuwa matumizi ya PASIPOTI yalianza mapema mwaka
1910 SOVIET UNION (URUSI) ndio walioanzisha kwa nia ya kuwathibiti raia
wao katika mfumo wa kikomunisti,baada ya hapo ndipo madola mengine yakafuata;
Leo tunapoongelea uraia pacha wengine wanachanganya pasipoti tu za kusafiria na kusahau haki za uraia na binadamu kwa ujumla.
Katika kanuni za haki za binadamu hairuhusiwi mtu kunyang'anywa uraia wake,
Mimi ningeshauri kuwa katiba mpya iruhusu raia watanzania waweze kuwa na pasipoti zaidi ya tatu,kwa sababu zitawasaidia katika maswala la maendeleo,kama vile uchumi,elimu n.k
MFANO HAI KUNA WATOTO WALIOZALIWA NJE YA NCHI  WAZAZI WAO WOTE NI WATANZANIA LAKINI WANAKOSA HAKI KATIKA NCHI WALIOZALIWA KWA KUWA SI RAIA WA NCHI HILE,NA WANAPOTIMIZA MIAKA 18 WANASHINDWA KUUKANA URAIA WA TANZANIA NA KUOMBA WA NCHI WALIOZALIWA JAPO NCHI WANAYOISHI WANAWEZA KUWA RAIA PACHA.
Watoto hawa wanasulubiwa kwa kuhukumiwa makosa ambayo hawajafanya ! kwani awakuomba wazaliwe ughaibuni,watanzania katika katiba mpya lazima tuwafikirie watoto hawa wasio na hatia.
Hata katika kanuni za haki za binadamu zinasema kuwa "Si ruhusa kwa binadamu yeyote yule kunyanga'nywa uraia wake.Sasa mtoto wa kitanzania
akiwa hana haki ya kuwa mtanzania kwa kuwa kazaliwa nje ya nchi ! hii si haki.
(B) Muwekezaji wa Kigeni anapokaribishwa Tanzania kwa maneno ya "Jisikie upo Nyumbani ! na mtanzania hakubaliki kwao hapa kidogo pana utata lazima patazamwe upya.

Kwa sasa kuna nchi nyingi duniani ambazo katika katiba zake zinasema kuwa raia wa nchi hizo harusiwi kuny'angwa uraia wake ata kama anaomba uraia wa nchi nyingine,sisi bado tunaogopa kulijadili kwa visingizio vya usalama.
Kwa Sasa hatuna adui kama ilivyokuwa zamani tuliofu makaburu n.k
Adui wetu wa sasa ni NJAA NA UMASIKINI na Uraia pacha unaweza kuwa silaha kubwa ya kupiga vita adui zetu hawa NJAA,UMASIKINI.

TUNAWEZA KUWEKA MASHARTI KWA WALE WATAKAO KUWA NA URAIA PACHA(Ras Makunja alisisitiza)
Mfano: Mtu akiwa na uraia pacha hawezi kugombea nafasi za juu ya uongozi wa taifa kama vile mbunge,diwani,rahisi.
Au kufanya kazi katika sekta ya usalama na mambo nyeti yanayo husu taifa.
huu ni mfano tu. Uraia pacha si swala la kuliogopa bali kuelimishana.

SWALI : MATEGEMEO YAKO ? KUHUSU KATIBA MPYA.

Ras Makunja: Ni mategemeo yangu kuwa wabunge katika bunge maalumu la katiba wataweka maslahi ya Tanzania na watanzania kwanza na kuondoa itikadi zao za ki-vyama kama tunanyoona sasa. Tunategemea watatuletea rasimu ya mapendekezo ya katiba yenye masilahi ya Taifa na watanzania kwanza
si vinginevyo. mwanamuziki huyo alimalizia.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake