Kocha mpya wa Simba, Mzambia Patrick Phiri
Kocha mpya wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, anatarajia kuwasili nchini leo kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuanza kukinoa kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara itakayoanza Septemba 20, mwaka huu.
Phiri anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mcroatia Zdravko Logarusic ambaye Jumapili wiki hii alitimuliwa na uongozi wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Simba, Evans Aveva, aliliambia gazeti hili kuwa tayari wameshafanya mazungumzo ya awali na Phiri na jana mchana walitarajia kumtumia tiketi ya ndege ya kuja Dar es Salaam.
Aveva alisema wameamua kumchukua Phiri kwa sababu ni kocha wanayemfahamu uwezo wake na anaifahamu pia Simba inachotaka kwa sasa.
"Pia anaijua Ligi ya Tanzania, nimeongea naye na amenikubalia kwamba yuko tayari kuja kufanya kazi na sisi (Simba), alisema Aveva.
Rais huyo aliongeza kwamba maamuzi ya kumtimua Logarusic yalizingatia mambo mengi na si kufanya vibaya katika mechi ya kirafiki iliyomalizika kwa Simba kufungwa mabao 3-0 na Zesco kutoka Zambia.
"Hatujakurupuka, ni maamuzi ambayo hayakufanywa kwa kuangalia matokeo ya Simba Day, naomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu wajue, kila tunachoamua ni kwa manufaa ya timu na klabu na si maamuzi ya watu binafsi," aliongeza Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kundi la Friends of Simba na Kamati ya Usajili.
Alisema wanaamini ujio wa Phiri utasaidia kurejesha heshima ya timu na klabu yao ambayo mwakani haina nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa.
Hata hivyo, kiongozi huyo hakuweka wazi ni mkataba wa muda gani watampa Phiri ambaye aliwahi kuipa Simba ubingwa wa Bara bila kufungwa mechi hata moja.
Baada ya Logarusic kutimuliwa, kikosi cha Simba kilibaki chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola ambaye anapewa nafasi kubwa ya kumsaidia Phiri kutokana na kuwaelewa vema wachezaji wa timu hiyo.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake