Tuesday, August 12, 2014

SAHIHISHO LA NAMBA YA WALIOPIGA KURA DMV KUTOKA KWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI

Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi, Bwn. Safari Ohamay akimwangalia kwa makini Alawi Omar anavyoweka kura yake kwenye sanduku
Mwenyekiti;

Rejea kwenye ripoti ya mada hapo juu. Mimi nilifanya makosa mawili: moja ni ya tarakimu; na nyingine ni kuhusu wanachama hai 150 waliotajwa. Tarakimu inahusu kura za Ismail Mwilima. Kura sahihi ni 173 badala ya kura 171 ambazo mimi nilikosea kuandika.

Kuhusu wanachama hai 150 nilimaanisha wale ambao hawakuja kituoni; siyo “waloamua kutopiga kura” kama nilivyoandika kwenye ripoti. Niwieni radhi.

Hivyo basi, wanachama ambao hawakupiga kura siyo 150, kwani watu 14 kati ya hao, japo hawakuja kituoni, walileta kura zao kupitia barua pepe na zilihesabiwa. Hivyo ni watu 136 ambao hawakupiga katika jumla ya wale 586.

Pamoja na hayo makosa ya tarakimu na ya kauli, matokea ya uchaguzi hayajabadilika na tamko la Kamati ya uchaguzi juu ya washindi inabakia kama ilivyotangazwa hapo awali.

Wenu Mtumishi
Safari Ohumay

Mwenyekiti wa Kamati

4 comments:

  1. Yale yale! "chicken come home to roost"

    ReplyDelete
  2. Dawa ni kurudia uchaguzi. Maelezo yote mnayotoa hayana mshiko.

    ReplyDelete
  3. tetetetete, yale yale ya mrema na slaa

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake