Karume amtembelea Mansour kituo cha Polisi
Zanzibar. Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume jana alifika Kituo cha Polisi Madema kumjulia hali shemeji yake, aliyewahi kuwa Waziri wa SMZ, Mansour Yusuph Himid ambaye alikamatwa na silaha mbili za moto na risasi 412, nyumbani kwake Chukwani hivi karibuni.
Karume alifika katika kituo hicho ambacho ni Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi saa 5.30 asubuhi na kumjulia hali Himid ambaye amewekwa mahabusu akisubiri uchunguzi wa polisi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.
Habari za uhakika kutoka ndani ya polisi zinadai kuwa Rais Karume alizungumza na shemeji yake kwa muda usiopungua dakika tano na kumtaka kuwa mstahimilivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na utaratibu wake.
Viongozi wengine waliofika katika kituo hicho ambacho kimeimarishwa ulinzi tangu alipofikishwa juzi, ni pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF; Hija Hassan Hija (Kiwani), Saleh Nassor Juma (Wawi), Hassan Hamad Omar (Kojani ) na Naibu Waziri wa Maji, Nishati, Makazi na Ardhi, Haji Mwadini Makame ambao walimpa mkono wa pole 6.30 mchana.
“Mansour anastahili pongezi na siyo kupewa pole, inashangaza mambo ya ulinzi na usalama ni ya Muungano kwa nini upande mmoja uruhusiwe kumiliki silaha na upande mwingine uzuiwe, ndiyo maana tunasema Zanzibar haitendewi haki,” alisema Hija muda mfupi baada ya kutoka kituoni.
Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi linapaswa kuendelea na operesheni ya kuwasaka viongozi wengine wanaomiliki silaha na kuwafikisha katika vyombo vya sheria kwa vile tukio hilo limewafunza mambo mengi na kutaka haki itendeke.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na matokeo yake ndiyo yatakayoamua wapi pa kufunguliwa mashtaka kati ya Zanzibar au Tanzania Bara.
“Kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, hairuhusiwi raia yeyote kumiliki bastola,” alisema.
Himid alipekuliwa nyumbani kwake juzi baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za kiintelejensia kuwa anamiliki silaha za moto.
Taarifa kutoka katika eneo la tukio zinaeleza kuwa kazi ya upekuzi wa nyumba mbili zilizopo katika eneo moja ilifanywa kwa kutumia mashine maalumu.
Chanzo: Mwananchi
Mansoor himid,aliyewahi kuwa mwakilishi na wakati flani waziri asiyekua na wizara maalum na pia ni shemeji wa rais karume,
Akutwa na silaha hizi
2 comments:
laahaula bwana mansoor hata kama hizo risasi za shortgun ni za kusakia, si utawamaliza hao paa wachache walioko zanzibar? na kwa risasi ulizokutwa nazo za bastola hao majambazi ungewamaliza hata kama wangekuwa batallion nzima. nakupongeza kwa kujipanga vyema kwa self defence.na sijui kama kina Tundu Lisu wangejitolea kuwatetea kama mlalahoi (low profile citizen)angekamatwa na idadi ile ya risasi na bunduki. hata hivyo tuacheni ushabiki wa aina yoyote ile. tuiachie mahakama ifanye kazi yake. kwa mtu kama mimi mzaliwa wa zanzibar na ninayeifahamu vizuri mambo ya kisheria si mambo yanayowasumbua sana viongozi wetu kwani kuna sheria nyingi tu zilizopitwa na wakati, mojawapo hii ya umilikaji wa silaha inahitaji marekebisho ili iende na wakati, lakini hawashughuliki kufanya marekebisho hawa akiwamo yeye mwenyewe alipokuwa mheshimiwa mansoor. as long as the law remaim in force is a good law, problem is many of us would say, but there are others who possess the fire arms illegally, who? we need proper amendments to some outdated laws particularly in zanzibar. matatizo ya kisheria ni makubwa mno bado.
hii picha mbona mmeikata mbona hatuonyeshi hizo risasi tuzione na tujadili katika blog yako hii mkuu?
unaficha nini picha nzima ? inaonyesha jinsi ccm walivyo magamba na mbubumbu mzungu wa reli.
bastoli mmojoa short gun wakati adam malima alimiliki zaidi ya hii na hairuhusiwe na serikali na ya pili ni silaha ya kuwinda ja ajabu nini?
inshallah Allah atakunusuru mansoour na njama za hawa magamba mbubuu wasioitakia mema zanzibar
Post a Comment