Iddi Sandaly ninasikitishwa na Liberatus Mwangombe kwa Maamuzi ya Kutoa mrejesho wa Swala zima la kukutana Muheshimiwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wa Washington DC.
Maswala yanayohusu utaratibu, Muda na usalama na Mahali ambapo mkutano unaomuhusu Rais Wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Hayako katika mamlaka ya Mtu yeyote zaidi ya Serikali Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania na Taasisi Husika.
Katika Jambo hili mtu yeyoyote hatakiwi kuwa na Degree au Diploma, hata Mtu wa Kawaida Haitaji ziada ya Mawazo kujua Hili.
Hii Inaonyesha Ni Jinsi Gani Bwana Liberatus Mwangombe anavyofanya Maamuzi na Anavyofikiria.
DMV KWANZA
Iddi Sandaly
Bofya soma zaidi usome barua ya mwaliko ilivyokuwa imeandikwa toka Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Marekani.
BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHI MAREKANI, MHE. LIBERATA MULAMULA, ANAWAALIKA WATANZANIA KUTOKA KWENYE MAENEO YA DMV PAMOJA NA MAJIMBO MENGINE HAPA MAREKANI, KUHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DR. JAKAYA KIKWETE, UTAKAOFANYIKA TAREHE 2 AGOSTI, 2014 KATIKA HOTELI YA MARRIOT, 1221 22ND ST NW, WASHINGTON DC 20037, KUANZIA SAA 12.00 KAMILI JIONI.
KWA WALE WATAKAOITIKIA MWALIKO HUU NA KUTAKA KUHUDHURI, WANAOMBWA NA KUHIMIZWA KUFANYA YAFUATAYO:
A. KUJIANDIKISHA MAJINA KWA VIONGOZI WAO WA JUMUIYA, MWISHO NI SIKU YA IJUMAA TAREHE 1 AGOSTI, 2014, AMBAPO VIONGOZI HAO WATAWASILISHA MAJINA HAYO SIKU HIYO IFIKAPO SAA 6.00 MCHANA, KWA NJIA WALIOKWISHAELEKEZWA.
B. KILA MSHIRIKI ATAPASWA KUWAHI SAA MOJA NA NUSU KABLA YA MKUTANO KUANZA, ILI KUJIPA FURSA YA KUTOSHA KUKAMILISHA TARATIBU ZA KUINGIA UKUMBINI.
C. WATU WOTE WATATAKIWA KUWA WAMEKETI UKUMBINI IFIKAPO SAA 11.40 JIONI. HAKUNA MTU ATAKAYERUHUSIWA KUINGIA TENA UKUMBINI BAADA YA MUDA HUO.
D. KILA MSHIRIKI ANAPASWA KUWA NA HATI YAKE YA KUSAFIRIA AU/NA KITAMBULISHO HALALI CHENYE PICHA YAKE KUTOKANA NA TARATIBU ZA KIUSALAMA.
KARIBUNI KATIKA KIKAO HICHO, FURSA MUHIMU AMBAYO KWA MARA NYINGINE MHE. RAIS AMETUPAPITIA TANZANIA DIASPORA
1 comment:
Kaka usipoteze muda, watu wengine hawana exposure wala hawaelewi jinsi diplomasia inafanya kazi so do not waste time kujibu. Yale yale,,,, badala ya mtu kupoteza muda kuandika GAZETI ya fiction thoughts maana hawa ndo ma-super star wa kuandika fiction thoughts kama magazeti!!! mtu mwenye akili angepiga simu ubalozi wetu na kuuliza haya maswali ili upate majibu. Mweeee akili ni nywele kila mtu ana zake wengine hawana, wengine wana kipilipili, wengine za kimanga. Msemo huu una ukweli ndani yake...
Post a Comment