Rais Kikwete, Mgeni
Rasmi katika Mkutano wa Diaspora
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Watanzania wanaoishi
ughaibuni (Diaspora) ambao umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014.
Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Diaspora Tanzania
(Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania
wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli
mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, wenye
kaulimbiu “Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza” (Connect, Engage, Inform
and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za uwekezaji na
ajira zinazopatikana Tanzania.
Imetolewa na: Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam
No comments:
Post a Comment