Mimi kama Mtanzania naandika hapa kuwaomba watumishi wa
Ubalozi wa Tanzania Washington DC ubadilike kuwa na hali ya ujamaa.Sisi kama Watanzania tunatakiwa kuwa na umoja kwenye kila jambo.Ubalozi mnatakiwa
kumshirikisha kila Mtanzania hususan katika shughuli za mikutano ya kijamii.
Huu ujio wa Raisi Kikwete na mwaliko wa kuwaita Watanzania
siku chache kabla ya huo mkutano umeonyesha wazi jinsi gani mnavyowadharau Watanzania wengine ambao wapo mbali kidogo na DMV au State za mbali.Wengi
wanajiuliza hivi Ubalozi wa Tanzania USA ni wa DMV tu?
Mualiko wa Rais hauwagi wa surprise sasa iweje nyie ndugu zetu
wa Ubalozi mtualike siku chache kabla.nyie kama wakazi wa hapa USA mnajua wazi
kuwa mtu anahitaji atleast 3 weeks au mwezi mzima ili aweze omba ruhusa kazini
au aweze kujitayarisha kivyake kuja kuhudhuria huo mkutano wa Watanzania wa
kuonana na Rais wao.kila mtanzania ana haki hio na Ubalozi upo hapa kwa ajili
ya kila Mtanzania sio tu watanzania wa DMV tu.Sasa kipi kilichawapa ugumu wa
kualika mapema?Hata huo msafara wa Rais ulihitaji muda wa more than two weeks
for visa processing etc.
Kingine ni kuhusu huo mwaliko wa wajasiriamali wa DMV
kukutana na Mama Salma, hivi naomba niwaulize lini mtaacha ubinafsi na ujamaa
wa kuitana wenyewe kwa wenyewe kuja msikia au munaona First Lady wetu.Hivi kwani Watanzania wengine au wanawake wengine ambao ni wajasiriamali pia hawana
haki?Sasa mbona hamjaalika kila mjasiriamali mwanamke?wa hapa USA. Hao
waliohudhuria ni wanawake wachache tu ambao mme wachagua kiujamaa jamaa na kiubinafsi.
Mwisho mimi kama Mtanzania mwenzenu naomba mbadili hii tabia
ambayo inagawanya watanzania na kuwafanya kujisikia vibaya kuwa wamebaguliwa
kisha kukata tamaa kabisa na ubalozi wetu.
Ni mimi Buhite Jabry
9 comments:
Nakubali kabisa na maneno ya hapo juu, especially huo mkutano wa akina mama ambao uliandaliwa na Tano ladies kushirikiana na ubalozi. Kama Tano ladies hawakupendi hata ukiwa mjasilimali wa hapa DMV you will never be invited. Ubalozi lazima muangalie mnaweza kuleta mgawanyiko mkubwa kutokana na issue binafsi za watu mnaowahusisha kuandaa shughuli na jina lenu likiwemo.
Muwe mnauliza siyo mnakuja tu mradi Marekani:( Marekani ni New York, La, DC..Sasa mnataka wote muualikwe kwani Rais amewatembelea WaTanzania? Rais yuko hapa kwa mualiko wa Obama kilichotokea ni ukaribu wetu wa kuwa D.C. Rais hakuitwa wala hakuja USA kutemblea WaTanzania..kama angekuwa Houston TX anaongea nanyi. .
Nakubaliana nawe kabisa wabinafsi sana ndio mahana hata utanzania siutaki wakae nao
Naungana na mtoa hoja.
Toeni taarifa mapema
Shirikisheni watu wote sio DMV tuu..
Na DMV acheni kutumia platform kama hiyo ukuweka siasa zenu kama jamaa alivyoomba kura .
Na pia mnatia aibu kuomba pesa za kufundishia watoto wenu kiswahili yaani pesa ya nchi iache kuboresha elimu ya kata ije kusaidia nyie ....rudini bongo kama mna njaa kiasi hicho.Nyie ndo mnafanya tuonekane wote wabeba box huku.Yaani mnashindwa kuchanga mkafanya daras la kiswahili kwa watoto mnapitisha bakuli shame on yuo DMV Community.
Anyway Ubalozi jueni kuwa USA ni kubwa si DMV tuu.Kiongozi anakuja ombeni mapema akutane na wabongo wa huku ughaibuni na tujulisheni mapema.
Ndugu mtoa mada Nakuunga mkono,hili walilofanya ni kosa, ila mama balozi ni jasiri sana na mpenda haki naamini atalifanyia kazi hili suala, basi tuwasamehe na tuwape muda wa kurekebisha makosa yalio tendeka.
Mdau asante sana, tatizo lako linaonekana haupo kwenye habari umeibukia kuzipata. Kila kitu kinakuwa kwenye utaratibu tu ni wewe tu sio mshirika na hata ungelipewa hizo wiki sidhani kama ungelijumuika kwa namna yeyote. asante.
Mdau, asante japo ninaona hapo umepoteza malengo sijui ulitaka uleteewe habari hizo mlangoni mwako kama unavyoletewa barua na posta usilemae kupata habari. pole saana.
Ukiwalaumu Ubalozi unakosea tu. Inategemea maamuzi mkutano utafanyika ama la yamefanywa lini na wakubwa huko nyumbani!! Ni rahisi kuwalaumu Ubalozi!
yap,nakuunga mkono ndugu yangu yaaani ni wabinafsi sijaona,unawaambia watu ghafla bin vuuu,wanakurupuka tu, hii ni America bwana hatupo Africa hapa,jaribuni kujali muda wa watu ati,am so pissed.
Post a Comment