Katika wadhifa wa rais kura zilikaribiana sana, na hivyo kamati ilionelea umakini katika kufanya ukaguzi wa ndani ili haki itendeke kwa kadiri ya uwezo wetu. Ukaguzi wetu ulizingatia maeneo hayo muhimu ya zoezi lote: 1) mfumo wenyewe wa uchaguzi kuanzia mlangoni mpiga kura anapoingia kwenye kituo hadi hatua ya mwisho anapotumbukiza kura yake kwenye masanduku; 2) wasimamizi waliohusika katika kila sehemu ya uhakiki;3) taratibu na jukumu la kuhesabu kura; 4)na utaratibu wa kutangaza matokeo.
1) Mfumo wa upigaji kura:
Mpiga kura anapofika kwenye kituo alijua masharti ya kutoa kitambulisho rasmi kinachomnasibisha na eneo la DMV. Katika sehemu ya kwanza anajitambilisha, kwa mtendaji wa kamati mbele ya mawakala; na wagombea wote walikuwa na jukumu la kuhakiki uhalali wa mpiga kura tarajia. Kila mpiga kura halali yuko kwenye orodha kuu ya wanachama hai. Na kama mtu haonekani kwenye orodha kuu, basi hawezi kupiga kura. Madhumuni pekee ya utaratibu huo wa kuwajibisha watu hao wote (mtendaji wa kamati, mawakala, na wagombea) ni kuondoa mashaka kwamba mmoja kati yao ataachia mwanya wa kuchakachua au kuharibu kura. Tunakumbuka kabisa wakala na wagombea wako pale kusimamia haki za mgombea husika, na kuripoti kitendo chochote pale kitakachoathiri uhalali wa kura.

2) Baada mwanachama hai kuchukuwa namba yake anaelekezwa kwenye meza nyingine iliyosimamiwa na watu wafuatao: watendaji wawili wa kamati, mawakala, na wagombea. Kwenye meza hiyo mwanachama anaonesha kitambulisho chake, na jina lake linawekewa alama na kupewa karatasi 5- moja ya rais, na zingine nne za makamu wa rais, katibu, makamu wa katibu, na mweka hazina. Baada ya kupokea hizo karatasi, mwanachama anaelekezwa kwenye jiko, ambako ni mahali pa kupigia kura za siri. Hapo kwenye mlango wa jiko, kuna mtendaji wa kamati, mawakala, na hata mgombea aliyejisikia kuwa pale. Mpiga kura anapomaliza kupiga kura huko jikoni, anaelekezwa kwenye masanduku manne yaliyopangwa kwa safu kwenye meza. Meza hiyo ya masanduku, ilizungukwa na: mtendaji wa kamati, mawakala makini, na wagombea wenyewe. Hapo kwenye masanduku alikuwa mpiga kura mwenyewe ndiye aliyetumbukiza hizo karatasi kwa kuzikunja na kusukuma: za rais na makamu wake kwenye sanduku moja, na zingine yaani za katibu, makumu wa katibu na mweka hazina katika masanduku matatu kila moja likiwa na bango la wadhifa.
3) Baada ya upigaji kura kufungwa mnamo saa nne hivi za usiku, utaratibu wa kuhesabu kura ulizinduliwa kwa shauku kubwa na ukaanza mara kwa kuhamisha masunduku kwenye sehemu nyingine yenye meza za kuhesabia kura. Sehemu hiyo ilizungukwa na: watendaji wa kamati wakisaidiana na wajumbe wa bodi ya DMV, mawakala na wagombea wenyewe. Maridhiano pia yalifikiwa kati ya wadau wote kwamba masanduku yafunguliwe na kura zote kumiminwa juu ya meza. Watendaji wa kamati wakishirikiana na wajumbe wa bodi walichambua bayana na kuwapa mawakala kura za wagombea wao. Baada ya kura zote kuondolewa mezani na kupokelewa na mawakala, hatua iliyofuatia ni kwa kila wakala, moja baada ya mwingine, kuhesabu kura alizopokea, alafu kutoa hiyo takwimu kwa mtendaji wa kamati/mjumbe wa bodi. Katika muda huo wote zoezi la kupiga kura lilipokuwa likiendelea wahusika wote walikuwa macho wazi, makini wakizingatia kuhakikisha hakuna wizi au uchakachuaji wa kura unafanyika. Hali hiyo ya shwari iliendelea bila malalamiko rasmi hadi baada ya matokeo ya hesabu za kura
Matokeo ya hesabu ya kura zote ambazo mawakala hao walitoa kwa kamati yalikuwa kama ifuatavyo:
Iddi Sandaly : 231; Liberatus Mwang'ombe: 214
Hivyo jumla ya kura zilizopigwa kwa rais pale kituoni ni 445. Kwa minajili ya kuhakiki kura hizo kamati ililinganisha hizo kura na idadi ya wanachama waliokuja kwenye kituo na kuchukuwa karatasi. Idadi yao ilikuwa 436 kwa mujibu wa namba zao na majina yao yaliyoainishwa kufuatia utaratibu uliotajwa hapo juu. Hah! Hesabu hazilingani na imekuaje? Hili swali liliibuka mara moja na likaamsha mihemko ya watu wakati muda wa kituo tuliolipia ulikwisha. Haikuwezekana kufanya tangazo rasmi ya mshindi bila kujibu hilo swali. Hivyo takwimu za awali zilitangazwa usiku huo ikifuatiwa na jukumu la kuchanganua hizo kura za masandukuni na wanachama waliopigia kura kituoni.
Siku iliyofuata kamati ya uchaguzi ilikutana ili kuhakiki:
1) idadi ya watu waliopiga kura kituoni. Orodha nzima ya watu 586 ililetwa na kuhakikisha tena namba na majina ya wale watu waliopewa karatasi za kupigia kura. Wanakamati wanne walikuweko na wengine wawili walitoa udhuru pamoja na kukabidhi ridhaa zao kwa kamati.
Matokeo ya ukaguzi wa kamati yalidhihirisha kwamba kuna tofauti ya kura 9 za ziada ambazo ziliingia kwenye masanduku. Imekuaje hizo kura zimeingia japo wakala, wanakamati na wagombea wenyewe wote walikuwa hapo? Jibu limebaki kwenye changamano hisia na tuhuma; hivyo inachakatwa kwa kuanza na nadharia-tete (hypothesis). Kama ifuatavyo:
1) kura hizo zilitumbukizwa na mpiga kura- yumkini yake ni asilimia 90 hadi 100;
2) Kura hizo zilitumbikizwa na mwanakamati, wakala, au mgombea- yumkini ni 0.
3) mpiga kura alipewa karatasi za ziada na mwanakamati- yumkini ni asilimia 90-100;
4) kuchakachua wakati wa kuhesabu- yumkini ni 0.
Kamati ilikiri kwamba wapiga kura wengine walipokea karatasi za ziada au walipokea karatasi 5 lakini za rais mbili hivyo kura moja batili.
Kwa jumla kura batili zilifikia 9.

Swali la Hitimisho: Je DMV inahalisi kusambaratika kwa ajili ya kura 9 batili? Je wale wanaopinga tamko la kamati lililotanzwa rasmi washindi wangejisikiaje kama wagombea waliopata kura chache ndiyo watangazwe washindi? Je hivyo si kusaliti demokrasia iwapo haikidhi matakwa yetu ya binafsi ?
Hitimisho: Makosa yaliyotokea yanaonyesha uzembe fulani kwa watu wote wahusika: Wanakamati/bodi, wagombea wenyewe na mawakala wao, na vile vile kwa wale wapiga kura ambao dhamira zao ziliwaruhusu kuingiza hizo kura kwenye masanduku: MSTAKABALI WA DMV NI MUHIMU ZAIDI KULIKO KURA 9 BATILI AMBAYO MIMI NAIHUSISHA NA “HUMAN ERROR”. W We have to learn to live with our human frailities without rupturing our well earned national solidarity that has become exemplary on the African continent. Mungu ibariki DMV na uimarishe mshikamano wetu.

Waongo wakubwa
ReplyDeleteNadhani ingefaa ukajitambulisha waziwazi ili hoja zako ziwe na mashiko pamoja na sura ya uwazi, ukweli na uzalendo unaojigamba nao. Kujificha utambulisho wako kunaopunguza kwa kiasi uzito wa hoja zako. Tujifunze kukubali makosa na kuyasahihisha badala ya kukimbilia hoja hafifu ya kukubali makosa tu eti kwa sababu ya kulinda "umoja na mshikamno" ambao unaweza kuwa feki!
ReplyDeleteSina Imani na junuia
ReplyDeleteKungekuwa na human error problems zingejitokeza kwa nafasi nyingine. This was a well calculated intentional act done knowing that election will be tight even a single extra vote would help. The whole election is a fraud. Let vice president lead for now and call for rerun
ReplyDeleteWe are tired of this Uchaguzi news,can we all get along and move on
ReplyDeletekwanza nampa hongera Libe pia namshauri mpiganaji anaekubali Libe aanzishe umoja wake kwani anao watu wakutosha..na wamuache Idd na hiyo kamati yake
ReplyDeleteNdugu mwandishi, ukiona kila wakati unaelezea jambo moja Mara kadhaa ujue kuna tatizo. Sijawahi kuona matokeo ya uchaguzi unakuja na hypothesis. Njia rahisi na ya haki ni kurudia uchaguzi.
ReplyDeleteKwanza jumuia itapata kipato kingine from monthly member contribution for the next month. Najua wengi walitoa ada ya mwezi mmoja tu. Sasa watalazimika kulipia tena ili wapige kura. Wengi watajitokeza tena na walio na nia ya kweli kuendeleza jumuia na mapumba yataonekana ambao walikuja kwa ushabiki tu.
Uchaguzi haukuwa sahihi,kura za maruhani zimeutia kinyongo.Kura moja ina count kama binadamu aliyeacha schedule yake na kudrive miles away ili kucast ballot yake.
ReplyDeleteUkaguzi na uhakiki huu umefanywa na Kamati ya Uchaguzi bila kuwepo wagombea au mawakala wao. Ikumbukwe kwamba, this is the very committee that failed our DMV Community, in the first place. How can one trust the outcome of an exercise carried out by a proven incompetent body? The so-called ukaguzi na uhakiki was nothing but a face-saving strategy. The only fair way to deal with this was to void the election results for the president's position because: (1) the difference between the votes recieved by each candicate was too narrow and no re-count was conducted in the presence of the candidates and/or their representatives (2) the existence of acknowedged fraudulent votes was by itself a sufficient ground for nullifying the election results.
ReplyDeleteShame upon you members of the Election Committee!!! You sold the DMV Community down the river.
na usiwe nayo who cares
ReplyDeleteMlioshindwa fire your wakala's wao ndiyo waliohesabu kura kwa mikono yao na wakatoa namba kwa TUME. LEAVE THE TUME ALONE.. WAMEFANYA KAZI NZURI HATA KURA 1 IKIZIDI STILL NI MSHINDI. TEAM LIBE YOU NEED TO GET ELECTION SPECIALIST AWAELIMISHE. Hizo kura mnazoziita za fradulent au zilizozidi ni 9 tu. Hivi hesabu mlisoma wapi?? Tofauti ya kura kati ya Libe and Iddi ni 13 HATA MALAIKA WAKISHUKA MATOKEO HAYAWEZI KUBADILIKA! OK MPE HIZO TISA LIBE KWA KUZITOA KWA IDDI STILL IDDI NI MSHINDI!!!
ReplyDeleteGET OVER IT! ACHA UTOTO...
hasira sio kura jamani ni hela walizowapa watu waje kupiga kura sasa wameshindwa imekula kwao. tetetetete,chichemi wala chimumunyi,mbona hizo comment kama zinatoka kwa yule mfuasi anayerekodi halafu baadaye anaomba msamaha. anzisheni umoja wenu kama mna ubavu.
ReplyDeleteBw Luke mbona umekalia kuandika matatizo ya jumuiya ya DMV tu huku twaambiwa NY napo moto unawaka? Waswahili hawataki amani wao ugomvi tu!!!
ReplyDelete