Mhe. Omar Mjenga leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya ENOC ya Dubai, Mhe. Saeed Khoory pamoja na uongozi wa juu wa kampuni hiyo.
Katika mazungumzo, wamejadiliana njia za kuongeza uwekezaji wa kampuni hii nchini Tanzania. Nia ni kuifanya Tanzania kuwa ofisi kuu ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Aidha, Mhe. Mjenga amemuomba Mhe. Khoory kuona uwezekano wa kampuni hii kuajiri Watanzania zaidi kuja kufanya kazi Dubai. Amekubali ombi hilo na kuahidi kutoa maagizo kwa idara ya ajira kuorodhesha nafasi zilizopo ili kuanza taratibu za kuajiri.
Kwa sasa, ENOC imekwishafungua ofisi zake Tanzania na wapo katika majadiliano na TPDC ili kujenga hifadhi maalum ya mafuta.
Mhe. Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Mhe. Saeed Khoory.
Picha ya pamoja na uongozi wa ENOC
Mazungumzo yakiendelea na uongozi wa ENOC
No comments:
Post a Comment