Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe (Picha na Maktaba).
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yafungiwe mara moja.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu muda mfupi uliopita, Dk Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu 39 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
“Ile sehemu ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na
daraja lipo katikati, kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na uzembe kama huu unasikitisha sana. Walikuwa wanaonana na hata lile gari dogo walikuwa wanaliona… hii hali inasikitisha sana,” alisema Dk. Mkwakyembe.
Alitahadharisa kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali ya kizembe ataaamuru vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya wananchi. “Katika uongozi wangu madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe mara moja wakisababisha ajali za kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.
(Habari na Elvna Stambuli wa GPL)
13 comments:
Sidhani kama kuifungia Kampuni ambayo dereva wake amesababisha ajali itakuwa ni kuwatendea haki kwa wamiliki wa makampuni husika.
Isipokuwa serikali itatakiwa kutokuwa wavivu na kuangalia root cause ya ajali hizi, baadhi ya sababu hizi ni
1.Rushwa katika kupata leseni za udereva.Hii inaondokea watu waiokuwa competent enough kukabidhiwa vyombo hivi na kuishia kusababisha ajali za kizembe.
2.Ulevi wa madereva, imekuwa kama jadi kwa madereva wa mabasi,malori ya mizigo kunywa pombe kabla na kila wakati wanaposimama katika vituo ya kupumzikia. etc.kunasababu nyingi ambazo serikali inabidi kuziangalia.Hili la Mwakyembe naona kakurupuka kutokana na jzba tu.
That's what am talking about, ACTIONS
Definitely yes, right action. Dr needs our support. Bravo Dr Mwakyembe.
Dk
Uk
NOPE, THAT IS NOT ACTION Anonymous # September 6, 2014 at 12:57 PM: That is a REACTION since it happens AFTER THE FACTS. On top of that these REACTIONS simply, will never help Tanzanians, since the Minister and others alike are aiming at Symptoms. Let Dr Mwakyembe and others know that ACCIDENTS are of some of the outcomes of POOR POLICIES and Overall POOR MANAGEMENT SYSTEMS that emanated from POOR LEADERSHIP.
Exactly… find root cause first and address that. Hizi abrupt reactions after the event hazitotupa lasting solution. Maisha ya watt TZ ni very cheap… watt wanakufa kirahisi na serikali haifanyi chochote kuaddress the reasons for silly deaths. I agree with the first commentator,
kufungia compuni husika sio suruhisho hata kidogo nacho fahamu mimi madereve wakitanzania hawapendi kufuata sheria suluhisho hapa ni kuanza kuwatrain wakina mama waanze kuendesha mabasi ya masafa malefu wakina mama wengi ni waoga kwavyovyote vile wataweza tu
Dr. Mwakyembe hajakurupuka yuko sahihi kabisa. Dr. Mwakyembe piga kazi bila wasiwasi kabisa, huo ndio utendaji bora. Tukipata majembe matano tuu kama wewe bongo itaendelea, na itatoka katika dimbwi hili la umaskini uliokithiri. Wamiliki wakifungiwa watajifunza kutafuta wafanyakazi / madereva wenye nidhamu ya kazi kama vile nchi zilizoendelea, pia ajali za uzembe zitapungua. Kazi yako inaonekana Dr , na kuna tofauti kubwa sana kati yako na wale waziri waliokuwa kwenye nafasi yako. Mungu akuongoze.
Kweli Mwakyembe kachemsha
Asante wadau. Ninakubaliana kabisa na mdau wa kwanza. Mheshimiwa Mwakyembe katoa yake, lakini serikali na yombo vya usalama viangalie hawa wapewa leseni kwanza na makampuni yawe yanaaajiri wale madereva waliofuzu na kufuata sharia za uendeshaji wa vyombo vya kubeba abiria na wawe wanaangaliwa kila mara. Unywaji wa pombe ni mojawapo pia kupata aleseni za kubebea abiria si ajabu kapewa tu..
Tunatoa pole kwa wafiwa.
Hizi ndio hatua ambazo tunazitaka ,mmiliki akiwajibishwa ,atawajibisha madereva wake, ni ngumu sana kwa serikali kucontrol dereva mmoja mmoja. kwa kufanya hv, madereva wataheshimu kazi zao na watakuwa makini, sababu Bosi hatakuwa tayari kuvumilia madereva wa namna hio
Dr Mwakyembe hajakurupuka kabisa, yeye yuko sahihi katika nafasi yake kama Waziri wa Uchukuzi, chapa kazi Dr maamuzi kama hayo ndio yaliyoleta maendeleo makubwa katika nchi zilizoendelea, pia bongo tunahitaji majembe kama wewe nasi ili tuweze kutimiza malengo ya 2025. Hao wadau wenye makampuni waliofungiwa ndio watajifunza na watakuwa mfano bora wa kuajili madereva bora sio bora madereva. Nao watakuwa na mchango mkubwa katika ushirikishwaji wa kubadilisha sera za nchi. Hayo mambo ya siasa za cause yatafanywa na Waziri wa sheria na katiba. Nchi zilizoendelea huwezi kusababisha ajali za kizembe za kupoteza maisha ya watu wengi namna hiyo na ukaachwa. Dr Mwakyembe uko sawa kabisa makosa yako kwa mwajiri na mwajiriwa.
Nakubaliana na mdau hapo juu serikali inatakiwa kutafuta root cause ya ajali but at the same time need to take action. Hapa mheshimiwa Mwakyembe atleast ametuma msg kwa kampuni nyingine za mabasi nina uhakika watawafukuza madereva wao watakao wabaini kwamba ni wazembe since hatakuwa tayari wafungiwe leseni zao. Kwa wale wenzangu mnaosema mheshimiwa kakurupa mnafahami fika ikiundwa tume kufanya uchunguzi hamna hata moja litakalo fanyika sana sana peaa zitaliwa na wana tume watapewa rushwa mwisho wake hamna yeyote atakuwa accountable. Atleast hapa kampuni hizo zimefungiwa badala ya kusubiri tume. Endelea na sera hiyo hiyo mheshimiwa
Kwa wadau wote mnaopinga, waziri yupo sawa Kabisa , ki sheria kila kampuni laZiwa iwe na Inservice kila baada ya miezi mitatu kuwafundisha wafanyakazi wao usalama barabarani , hiyo ni laZima , Kama dereva kashindwa , basi atolewe Kazini, kwa hiyo hizo kampuni hazikuwapa "safety first" wadereva wao ,huo ni mfano kwa waliyobaki ,, dereva afundishwe usalama na kampuni. Ndiyo maana katoa hiyo hukumu .. Mtoto akikosea shule nani anaitwA ?
Post a Comment