ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 8, 2014

JESHI LA POLISI LAKAMATA BUNDUKI NA MABOMU TUKIO LA UJAMBAZI KITUO CHA POLISI BUKOMBE

 hizi ni baadhi ya  siraha zilizokatwa baada ya uperesheni kali ya jeshi la polisi wilayani bukombe kufanya opereshi hiyo .


 hizi ni badhi ya siraha zilizokamatwa na jeshi la polisi wilayani bukombe  mkoani Geita baada ya askari wawili wa jeshi hili kupoteza maisha .

 kituo cha polisi ushirombo ambapo kilivamiwa na majambazi na kupoteza askari wawili na majambazi hao

Wakazi wa mji wa vitongoji vya Bukombe mkoani Geita na maeneo jirani wakiwa katika kituo cha Polisi Bukombe kuaga miili ya askari wawili waliouawa kwa bomu juzi usiku baada ya majambazi kuvamia kituo hicho na kuwashambulia kisha kupora silaha. Picha na Ernest Magashi

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa jeshi la polisi mkoani  Geita limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu 10 eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe.

Inasadikiwa kuwa bunduki hizo ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  usiku wa kuamkia jana. 




Bunduki hizo, nne zikiwa SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuru la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.


Habari zinasema kuwa  katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi linaloendelea kufanya kazi nzuri  limemkamata  pia mwalimu mmoja katika shule ya sekondari Ushirombo anayedaiwa kushiriki katika tukio la jana.


Tayari watu wengine watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi.
imearifiwa kuwa  jeshi la polisi linaendelea kufanya msako ili kuwakamata wahusika wote na silaha zote zilizoporwa na majambazi hao. 

No comments: