Ndugu Watanzania Wote Wana DMV. Uongozi Unapenda kuwajulisha na Kuwaomba mje kwenye Mkutano mkuu wa jumuiya utakaofanyika
Jumapili September 7, 2014, saa 11 za jioni(5:00PM).
Jumapili September 7, 2014, saa 11 za jioni(5:00PM).
Indian Spring Terrace
9717 Lawndale Drive
Silver Spring, MD 20901
Agenda Kuu za Mkutano ni :
1. Kujadili Katiba ya Jumuiya
2. Kuungalia muelekeo wa Jumuiya Yetu.
3. Report Ya Fedha
4. Haki ya Kuzaliwa-Uraia Pacha
4. Haki ya Kuzaliwa-Uraia Pacha
Tunawaomba wote muipitie katiba ya Jumuiya na mje na haya:
1. Kipengele cha Kurekebishwa na Kirekebishwe vipi.
2. Kipengele cha Kuongezwa na Kwa nini.
3. Mengineyo
Tutajadili Katiba na Kupeana muda mwengine na kitaitishwa kikao kingine baada ya maoni kupitiwa na wana DMV wote.
Katiba inapatikana chini ya page hii : http://watanzaniadmv.org/about.asp
Kama unaswali lolote au ushauri wasiliana na ;
Email ni: info@watanzaniadmv.org
Rais- Iddi Sandaly @ 301-613-5165.
Makamu wa Rais- Harriet Shangarai @ 240-672-1788
Makamu wa Rais- Harriet Shangarai @ 240-672-1788
Katibu- Saidi Mwamende @ 301-996-4029.
Makamu Katibu- Bernadetta Kaiza @ 240-704-5891.
Muweka Hazina- Jasmine Rubama @ 410-371-9966
Muweka Hazina- Jasmine Rubama @ 410-371-9966
10 comments:
Rais na timu yote ya uongozi asanteni kwa taarifa. Na mimi nintaingia kwenye kamati mbona kina mama wanajitolea mambo mengi?? Halafu mnawatukana. Kina baba tupunguze vilabu na mabilauri ya pombe tujumuike kuijenga jumuiya yetu...
Kazi nzuri, na nyie mnaolalamika kuwa jumuiya ina udini njoo ujiunge na Jumuiya Rais ametangaza hadharani anatafuta wanakamati sio wakitokea wa dini moja muanze kupiga domo!!!!!!!!
LETS GO GUYS!!!!!!!!!!!!!
Tunakutania wapi?
Mnataka kubadiri katiba ili mdumu milele siyo?
Mkutano utakuwa wapi, hiyo siku ya Septemba 7?
Dj LK, Mbona mwaficha comment nyinginezo haziko wazi, Kama ya USIKU WA JAKAYA MMEIFICHA. Ninyi mnaoana raha kututangazia kuja kula wakati mnaona wazi kabisa ameshindwa kutetea katiba mpya nahata lile la Raia pacha amelikomalia kiasi cha uhamiaji kulitupilia mbali. Sasa mnataka tuje kula naye ya nini kama kupewa si amepewa kwa kutumaliza.. tuwe wastaarabu.
Aisee, ninakubaliana kidogo na msemaji wa hapo juu. Swala la kukataliwa kwa uraia pacha lawama nyingi sana tuzipeleke kwa rais wetu Mh. Kikwete. Rais Kikwete alipokwenda Washington DC baada ya kuulizwa kuhusu hili swala la uraia pacha, alijibu kuwa sisi Watanzania tunaokaa nje tunatakiwa tuongeze juhudi ili uraia pacha upitishwe. Wakati huo akijua kabisa kuwa hatukuwa na sauti yenye nguvu kule bungeni ya kuweza kuleta mabadiliko. Alipokwenda London alisema maneno hayo hayo. Alipokwenda San Rafael California aliseama maneno hayo hayo. Na mwisho hivi karibuni aliporudi Washington DC hakubadilisha kauli yake. Ukweli ni kwamba yeye rais wetu angetaja kuwa ni wazo zuri, lingeweza kupita, lakini hakutaka uraia pacha upitishwe.
Sawa kabisa msemaji wa hapo juu. Tunasherehekea nini na JK kama hata kutupigania tupate urai pacha ameshindwa? Tunafungua matawi ya CCM na CHADEMA lakinin wnzetu nyumbani hawatutaki mbali na misaada kibao tunayopeleka kwa ndugu zetu na kuinufaisha nchi. Can we real say we want to join him and congratulate kwa kazi bora aliyofanya? Open comment kwneye lile tangazo la dinner ya JK ndio utakapoona feelings za wana wa Diaspora...
The guy is not in favor of dual citizenship. Alishawahi kuuliza, namnukuu "Sasa ninyi mnataka kula huku na huku....?" Then he turned his question into a joke, hakuna aliyecheka. Sisi tuchukue urai wetu wa magharibi kilaini ili tusaidie familia zetu. Tena kama upo US, bongo unaenda kiulaini bila viza unaombea pale airport Dar/Kilimanjaro ambayo ni guarantee kupewa. Ukitaka passport ya TZ kwajili ya kunulia viwanja/mashamba unapata kiurahisi sana.
Naomba mfungue comment kwenye usiku wa jakaya please watu wana yao machache
Maoni mengi yamepelekwa kwenye lile tangazo la Usiku wa Jakaya naona yamezimwa. Afadhali mfunguwe ili mpate kupima joto, la sivyo mtapata aibu kumleta Rais hapa na asipate watu wa kujitokeza. Watu wana dukduku kwa nini tunakwenda kumpongeza wakati yeye kama Rais na kiongozi wa Chama Tawala hajatusaidia kilio chetu cha kupata Uraia Pacha. Mbona suala la serikali mbili amelikomalia na kushinikiza kinyume na Tume ya Warioba, kwa nini hili linammshinda? Je huo si unafiki?
Post a Comment