Pichani msanii wa siku nyingi aliyejizolea umaarufu kwa kucheza na Nyoka Bi Salima Moshi [Mama Nyoka ] Akiwakilisha Taifa Nchini Zambia kwenye maonyesho ya kibiashara ya kimaTaifa yaliyofanyika Lusaka
Sisi wasanii tulio nje tunawaunga mkono kwa dhati juhudi kubwa kabisa mnazofanya kupambana Kufa na kupona kufunga safari hadi Dodoma Bungeni kuhakikisha katiba mpya inatutambua wasanii kama kundi maalumu na kupata wawakilishi wetu ndani ya Bunge watakaoweza kuwasilisha hoja zetu na na kuhakikisha zinapitishwa maana msanii ndiye mwenye kujua uzito wake kama waswahili wanavyosema "Uchungu wa mwana aujuaye Mzazi " pia na kuweka sheria ya kulinda mali za msanii zinazoshikika na zisizoshikika [miliki bunifu] nawapongeza kwakuweza kukutana na wabunge mbalimbali kukutana na Mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba MhSamuel Sitta na kukutana na Waziri Mkuu MhMizengo Pinda Bungeni Dodoma Hakuna abishae kuwa wasanii wengi wamekufa masikini kwa kutokuwa na wawakilishi wakusimamia haki zao zinalindwa kisheria na kunufaika na kazi wazifanyazo kuna wasanii wengi ambao wamekwenda mbele za haki lakini si watoto wala familia inayonufaika na jasho alilolitoa kwamfano Mbaraka Mwinshehe Salum Abdallah Hemedi Maneti Marijan Rajabu[Jabali la muziki] TX Moshi Wiliam Mzee Moris Nyanyusa [Ngoma yake ilikuwa kiashirio cha Taarifa ya Habari] Bi Kidude mzee Mwinamila[Alizunguuka Tanzania nzima na Mwalimu] Mzee Issa Matona Kuna wengi ambao hawakuweza kufaidi matunda ya kazi zao hata familia zao hivi majuzi tu mzee wetu Marehemu Muhidini Gurumo alipewa gari na Mwanamuziki Diamond ambaye sawa na mjukuu wake muda mfupi kabla ya mauti kumfika akiwa amepiga muziki kwa zaidi ya miaka 40 hebu tujiulize amefaidika kweli na kazi ambayo ameitumikia kwa maisha yake yote Ukiangalia huku Marekani Msanii kama MICHAEL JACKSON Hadi leo familia yake inanufaika na jasho lake naunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Mashirikisho ya Sanaa NchiniTanzania Kupigania haki ya Msanii
No comments:
Post a Comment