Kikosi cha kwanza cha Simba kilicho anza hii leo taifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Na Beatrice Mroki-Taifa Dar es Salaam
AKIWA anaijua vyema timu yake ya zamani ya Gor Mahia ya Kenya, nyota mpya wa kimataifa wa Simba ya Dar es Salaam, Raphael Muigai Kiongera 'Modo' leo ameiongoza Simba kushinda goli 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa jioni ya leo.Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na nyota huyo aliyesajiliwa kutoka Gor mahia ya Kenya, Raphael Kiongera alkiingia kipindi cha pili akitokea benchi na bao moja kuwekwa wavuni na Ramadhan Singano 'Messi'.
Simba imetoa kichapo hicho ikiongozwa na kocha wake wa mara ya tatu, Mzambia Patrick Phiri ambaye alikishusha kikosi hicho uwanja wa taifa jiji Dar es Salaam ikiwa ni takriban mwezi na siku kadhaa tangu ilipo pata kichapo cha goli 3-1 na kupelekea kutimuliwa kwa kocha Zdravko Logarusic kutoka kwa Zesco United.
Kiongera alipachika goli dakika ya 55 wakati goli la pili likifungwa dakika ya 74 na Messi na Kiongera tena kufunga hesabu katika dakika ya 78.
SIMBA ILIWAKILISHWA NA
Ivo Mapunda, Miraj Adam, Abdi Banda, Hassan Isihaka, Owino Joseph, Willium Lucian, Awadh Juma, Shaban Kisiga,Elias Maguri, Emanuel Okwi na Ramadhani Singano.
Benchi la akiba walikuwepo Hussein Sharif, Manyika Petter,Mohamed Hussein, Nassoro Masoud, Abdalah Omar, Ibrahim Twaha, Uhuru Seleiman, Abdul Makame na Raphael Kiongera.
Benchi la ufundi alikuwepo: Kocha MkuuPatrick Phiri, kocha Msaidizi, Seleman Matola, Meneja wa Timu, Nico Nyagawa, daktari, Yasin Gembe, Kocha wa Makipa Idd Pazi 'Father' na mtunza vifaa Ngade Ngalembe.
No comments:
Post a Comment