ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 5, 2014

WANADMV ENDELEZA UPENDO NA UKARIMU KWA WATOTO YATIMA TANZANIA .







Wapendwa  WanaDMV Jumuiya yetu inatuomba kuchukuwa fursa kututambulisha  uwepo wa Sister Maristella Wamtende ambaye ni  mkuu wa Kituo cha watoto yatima kilichopo Sumbawangani mkoani Rukwa.
Kituo hicho kina  watoto wadogo wapatao 86 ambao baadhi  huokotwa vichakani, chooni na wengine hutelekezwa mbele ya milango ya kituo  wakiwa na umri wa siku moja. Vile vile kituo hicho kina shule ya msingi na Sekondari yenye  wanafunzi wapatao 500.

Baadhi ya changamoto zinazokabili watoto hawa ni pamoja na ukosefu wa maji,chakula,mavazi na hata usafiri hasa inapohitajika huduma ya tiba ya dharura.
Ndugu WanaDMV, TUENDELEZE UKARIMU NA UPENDO WA DHATI KWA TAIFA LETU, tunaomba tujitokeze kwa wingi kusaidia na kuwapa upendo watoto wetu, kwa kujitolea kwa nguo, viatu, vitabu, madaftari, kalamu mahitaji ya huduma ya kwanza kama gloves,bandage, gauze au  chochote  chochote ambacho kitawasaidia watoto na ndugu zetu.

Mchango huu utakusanywa katika anuani ifuatayo;

Indian Spring Terrace
9717 Lawndale Drive
Jumapili September 7, 2014, saa 11 za jioni(5:00PM).

Sister Mariastela
210-589-3590 au 443-518-6446
Anuani;4203 Wilkens ave, Baltimore MD 21229.

Tunatanguliza shukrani   kwa niaba ya kituo cha watoto Sumbawanga.

ASANTENI SANA
Uongozi


No comments: