Friday, October 10, 2014

Ally Kheir Daxx: Nyota ya Kitanzania inayong’ara Afrika

DAXX: “Nilifika pale kwa ajili ya kumpa sapoti rafiki yangu, Mtanzania mwenzangu, mbunifu mahiri Shera Ngowi, aliyekuwa akishiriki katika onyesho hilo.” 
Safari ya staa huyo kama ilivyo wanamitindo wengine nchini ilianzia kwenye maonyesho ya Swahili Fashion Week. Yalipofanyika kwa mara ya kwanza nchini, yeye na wenzake walikuwa vinara waliofanya vizuri kwenye ndani ya ukumbi wa Diamond Jubelee jijini.

KWENYE orodha ya wanamitindo wanaofanya vizuri kwa sasa barani Afrika huwezi kulikosa jina la Ally Kheir Daxx. Kwa wale wanaofuatilia matangazo ya runinga nchini, sura ya kijana huyu si ngeni machoni mwao. Kwani amekuwa akitokea kwenye matangazo mbalimbali ya biashara.


Safari ya staa huyo kama ilivyo wanamitindo wengine nchini ilianzia kwenye maonyesho ya Swahili Fashion Week. Yalipofanyika kwa mara ya kwanza nchini, yeye na wenzake walikuwa vinara waliofanya vizuri kwenye ndani ya ukumbi wa Diamond Jubelee jijini.


Katika mtiririko huo, Ally alishiriki katika maonyesho hayo, akiwa kioo kwa wanamitindo wenzake. Kwani kupitia yeye wavulana wengi waliingia kwenye uanamitindo na kumtumia kama mwalimu wao.


Baada ya kufanya kazi za kuonyesha mavazi pamoja na matangazo mbalimbali, Ally alikwenda Afrika ya Kusini kuhudhuria onyesho la Mercedez Benz Fashion Week Afrika lililofanyika jijini Johannesburg.


“Nilifika pale kwa ajili ya kumpa sapoti rafiki yangu, Mtanzania mwenzangu, mbunifu mahiri Shera Ngowi, aliyekuwa akishiriki katika onyesho hilo,” alisema.


Tangu wakati huo amekuwa akipata kazi mbalimbali na hivyo kuamua kuweka makazi yake nchini humo.


Sasa Daxx Hans amekuwa akipamba majarida mbalimbali ya mitindo ndani na nje ya Tanzania hususani Afrika ya Kusini. Baadhi ya majarida aliyowahi kufanya nayo kazi ni pamoja na FAS, Sawubona,Denstiny Man, Bhang na Drum .


Ukiachilia mbali ushiriki wake kwenye maonyesho ya mitindo nchini Afrika Kusini na nje ya nchi hiyo, Mwanamitindo huyo amekuwa akishiriki kwenye kampeni za kutangaza mavazi yanayotengenezwa na makampuni makubwa nchini humo. Baadhi ya kampuni hizo ni Mr Price, Edgars, Zara na Markham.


Kwa upande wa mavazi yeye binafsi hupendelea kuvaa mavazi yaliyo kwenye chati. Lakini pamoja na hilo anapenda kuvaa kile kinachomuweka huru.


Akizungumzia mafanikio yake Ally anasema, kujituma ndio siri pekee ya kupiga hatua katika maisha yake. Kwani siku zote amekuwa akiamini, hakuna njia rahisi katika kufanikiwa. Ili mtu afike huko anatakiwa apambane.

Umeshawahi kuona mitindo yake, mfatilie. Credit:Mwanaspoti

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake