ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 21, 2014

LUNDENGA AMTETEA MISS TANZANIA 2014 KUHUSU SAKATA LA UMRI WAKE

Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo 

"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.

Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wakazazi wake.
Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.
Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa habari. video ya alichokisema Miss Tanzania itawajia muda si mrefu. 

Habari na picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto

5 comments:

Anonymous said...

Kweli huyu Tanzania ni ,muongo akae pembeni ,hata kuongea anababaika

Anonymous said...

ukisikia bongo ndo hii.

Hamna kitu hapa mimi nadhani ushindi kapewa tu maana maswali yote alio ulizwa amekataa kujibu sasa nashindwa kuelewa na maswali yalikuwa rahisi sana ila poa hamna neno kama haki ni yake sawa Mungu ambariki na kama haikuwa yake pia sawa haki inatolewa na Mungu na sio mwanadamu kwa maana mwanadamu anaweza kutengeneza mazingira yatakayo kufanya uonekane una haki wakati haukustaili kuwa na haki hiyo ni hayo tu.

bwana jamaa kapewa unyumba hapo ndo maana..haha haha

Do blood test to find out the truth age

Anonymous said...

Eti ni
I kuwa sijajiandaa kujibu maswali yenu. Sasa kitu cha ukweli lazima ujiandae jibu Si utakuwa nalo. MISS GANI HADIEJIBU MASWALI ANAKUWA MKALI NA KUDENGUWA, KWANI MTU UKISAFIRI SAFIRI NDO UNAPOTEZA CHETI.???. Hicho Cheti Si mipya???? Kwa mahana hiyo police report ni mpya TAJA POLICE GANI ULIENDA. Mbona umeshindwa kujibu ili ushushue haters wako bana. Hii kitu imepikwa. DJ usiminye twafadhari Asante .

Anonymous said...

Mamaaa huyu miss mbona mzee kakomaaamose na nyoooooo Kama hizo hazifanyiwi na 23yrs old we umekubuhu bwana LUNDENGA MVUE UMISS la sivo ataje alienda police gani au mnaenda kuhonga kituo cha police ndo mkitaje. MISS TANZANIA COMMITTEE IMEPATWA LAANA YA PATEL. HONA MNAVOUMBUKA HILO LIMAMA ZEE LA DALS TX LIVULIWE TAJI ASAP

ASANTE DJ LUKE

Anonymous said...

lundenga atamvuaje u miss wakati yeye ndo anayemtetea.someni nyakati ya mambo yanavyokwenda na kupikwa bongo land