Thomas Eric Duncan aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola huko nchini Liberia ,alikuwa amewekwa katika karantini katika hospitali moja ya mjini Dallas ili kupewa dawa za majaribio.
Awali ,Marekani ilitangaza masharti mapya ya usalama katika viingilio vyote vya taifa hilo ili kuwakagua wasafiri walio na dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3000 wamefariki na wengine 7500 kuambukizwa wengi wao kutoka Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Ebola.
Huku Dancun akiwa raia wa kwanza nchini Marekani kupatikana na ugonjwa huo,raia watatu wa Marekani pamoja na mpiga picha mmoja waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo nchini Liberia.
Habari hizo zilijiri mda mchache tu baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry kutoa wito kwa mataifa yote kuimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugonjwa huo. BBC
6 comments:
ukiona mwenzaka kanyolewa nywele na wewe tia maji kichwani huwezi jua lina utakuja na wewe kuja kunyolewa hizo nywele zako.
ushabiki wa kushabikia vyama vya siasa huko majuu sasa si mnaona wasivyowajali watu weusi.
Nilikuwa nafuatilia eti walisema kwamba wazungu walio pewa dawa hiyo madoctor wao waliomba yeye hajaomba apewe na hata hivyo ile dawa imewaishia. na inachukua muda kutengeneza inginewe..hivyo alikuwa hapati treatment yoyote...mmnnnhhhh
Yani mpaka nikahisi labda wamefanya kumkomoa ili isije kuwa trick watayotumia wengine kama yeye kusafiri kwenda nchi kama US kupata treatment...
Thomas Eric Duncan lay sick in his hospital bed for nearly six days before the hospital tried a different experimental medication.
and he was given dawa aina ya brincidofovir badala ya Zmapp waliowahi wazungu walioumwa ebola, Matokeo wazungu walipona kwa Zmapp na baadae yeye mtu mweusi;mwafrica mwenzetu alikufa baada ya kutumia brincidofovir
mungu amlaze mahali pema peponi.inasikitisha sana,ni mwafrica mwenzetu na huu ugonjwa umetengenezwa kutuangamiza sisi waafrica.
wamemwacha afe kwa vile ni mweusi na ni Mwafrika.
Kwahio braza, kubali tu kuwa huko marekani when push comes to shove wewe mweusi tena raia wa kufikia mbeba ma box uko last on the pecking order. Hawezi akaachwa mzungu mwenye kazi yake ya maana kupewa dawa uakpewa wewe. It's a tough pill to swallow, but yes brother they lied to you when they told you all men are equal! Pole!
Chalii walimnyima dawa. Hamshangai wale wazungu walioumwa ebola wote walipona?. Alipoenda mara ya kwanza hospital aliwaambia katokea Liberia na isije ikawa ana ebola,madokta wakampuuza wakampa anti bakteria wakamwambia nenda nyumbani! Na isije ikawa huyu aliwahishwa kuondoka ili asiambukize wengine
Post a Comment