Cassim Mganga akipata ukodak na shabiki wake Simba Sakapala alie msindikiza uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Dulles tayari kwa safari ya kurudi Tanzania. Cassim Mganga alikuwa Marekani kwa Mwaliko maalum na namba moja blog Marekani Vijimambo kwenye sherehe zake za kutimiza miaka minne toka blog hiyo kuanzishwa.
Cassim alikuja na Aunt Ezekiel maalum kwa shughuli hizo za Vijimambo zilizo kuwa zimefanyika tarehe 13 mwezi wa tisa na Aunt Ezekiel aliwahi kuondoka na kumuacha Cassim kwa ajili ya kuhudhulia mkutano wa Dicota uliofanyika North Carolina mwanzoni mwa mwezi huu.
Vijimambo Blog ni kawaida yake kila mwaka uwaletea watu maalufu kutoka popote Tanzania na kujumuhika katika sherehe zake.
Tega sikio mwaka ujao nani atakuja au kama una wazo basi unaweza kuwakilisha kupitia chumba cha maoni na vijimambo itapitia na kufanyia kazi ombi la wapenzi wake kwani tunawajari na tungependa kuwafurahisha pale inapowezekana.

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake