Saturday, October 11, 2014

TANGAZO KUTOKA TAWI LA CCM NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE

 Tangazo kutoka kwa Mwenyekiti wa tume huru ya kusimamia uchaguzi wa chama tawi la New York na vitongoji vyake Bwana Isaac Kibodya na wajumbe wenzake walikutana kupitia taratibu zote za uchaguzi Na kuafikiana kupitisha majina yafuatayo kwa uchaguzi wa Jumamosi October 11, 2014 Katika nafasi ya Mwenyekiti wagombea ni Bwana. Sefu Akida na Bwana. Maftah Hassan. Mweka hazina ni bwana. Henry Stambuli. Umoja wa vijana walioomba nafasi ni Mr. Gastol Mkapa na katibu wake ni Bi. Bahia Maundi. Katibu Mwenezi na Siasa Bwana. Steve Bubelwa na wajumbe wanaogombea nafasi za ujumbe wa halmashauri kuu ya tawi ni Bwana. Ernest Magawa, Mr. Maurus Mwingira, Bwana. Shabani Mseba na Bwana. Ibrahim Selungwi. Tume imeunda mwongozo ambao utawatangazia wanachama ili zoezi hili la kuchagua viongozi liwe la haki kwa wote siku ya uchaguzi. Kwa niaba ya wajumbe wenzangu Bi Joyce Mkapa, Bi. Hamisa Maundi ( Prof Luiza alitoa udhuru) na Bwana. Justin tunatoa shukran nyingi na kuomba ushirikiano wenu wa Hali ya juu siku ya uchaguzi,  uchaguzi huo utafanyika Mt Vernon Address hii:
30 Overhill Road, 
Mt. Vernon, New York
 kuanzia saa nane mchana siku ya Jumamosi ya tarehe 11 mwezi huu wa kumi kabla ya uchaguzi wagombea watajinadi kwa wapiga kula sambamba na music, kujipati vinywaji na chakula. Nyote mnakaribishwa.  Mungu ibariki Tanzania, CCM Oyeeeee.
Baada ya uchaguzi watu watajimwaga kwenye Lounge ya Alomo kusakata rumba kuwapongeza viongozi watakaochaguliwa. Kwaiyo jiandae kwa Mduara kwani kiingilio ni miguu yako tu Alamo hadi joogoo afungue mlango.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi leo hii huko Mt Vernon Bwana Isaac Kibodya

14 comments:

  1. TUNAHURU KWA HAYO. NA MAHITAJI SI VIONGOZI TUU BALI NINGEZIDISHA KUSEMA VIONGOZI WAADILIFU WA CHAMA. WALIKUEPO NA TUNATAKA WAWEPO NDANI YA UONGOZI UJAO.TUNAWATAKIA KILA LA KHERI WAGOMBEA.

    ReplyDelete
  2. Mambo ya vyama hayo mngerudi bongo Hayana mpango hapa

    ReplyDelete
  3. TUNAJUA MTACHUKIA LAKINI TILITHUBUTU NA TULIWEZA NA TUNAENDELEA.CHURA HAMKATAZI N'GOMBE KUMYWA MAJI MTONI.....

    ReplyDelete
  4. Wapi shabani mseba! ?tupeni taarifa plzz

    ReplyDelete
  5. Hawa wameletwa hapa na wazazi wao na huletewa pesa kutoka Tanzania ndio maana hawana kazi za kufanya

    ReplyDelete
  6. umenena sadakta mdau wa mwisho ukiwaona watu wameshughulikia mambo ya chama chama ujuwe either wameletwa na wazee wao na pesa wanaletewa kutoka bongo,wazee wao wako serikalini wanaletwa mpaka wake zao huku kwenye misafara ya raisi na pia ukiwaona hawa ujuwe pia lazima wataipenda ccm imewasaidia sana hichi chama.

    yote kheiri laki haina nome so kama wenzangu hajaletwa na wazazi wenu au hamna mtu bongo anakuleteni pesa basi tafakarini na maisha ya hapa.

    vyama vya wapeleke bongo wanaoshabikia vyama hapa huwa wanapata mradi wao mambo swafiii yanawanyokea ndo maana wanapigia debe vyema.

    na shabani msebe yupo walipo watu wajanja wanapokuwepo.mwenzenu mtoto wa mujini mambo yake ya mujini lazima atakuwa anaishi na watu wa mujini.

    hawewezi watu kukupa taarifa yake hawa wanaogopa.

    nawakilisha na nimefurahi kwa comment za wenzangu.

    marekani piga kazi soma kwa bidii ukipata nafasi mambo ya chama wachiyeni wenyewe watoto wa chama msije mkaukweya mkenge kutoka ikawa balaaa kama shabani msebe.

    ReplyDelete
  7. Rais Kikwete msaidie Shaban Mseba walau arudi Bongo. Nadhani huko aliko anahitaji msaada

    ReplyDelete
  8. kwani kasema anataka kwenda bongo huyo shaban mseba,kihere here cha nini kwani mmesikia yupo wapi? umbeya tu umekushikeni.

    ReplyDelete
  9. raisi hawezi kumsaidia muhalifu. pinga

    ReplyDelete
  10. WA TANZANIA WENGI WANAPO FIKA MAREKANI WANAJIONA WAO NI WA JANJA AU WANAJUA ZAIDI WANAANZA KUTOA SHERIA KWA NDUGUZAO WAFANYE NINI HALAFU WANAJISAHAU WANAANZA KUTOA SHERIA KWA WATU WASIO WAHUSU KAMA KUNA KITU NATAKA KUFANYA NAWEWE WAKIONA HAKINA MAANA YAKUHUSU NINI NYAMAZA WATANZANIA TUNAO UHURU KUFUNGUA CHAMA CHAINA YOYOTE HAPA MAREKANI WEWE NINANI KUWAAMBIA WARUDISHE VYAMA NYUMBANI AU HATUTAKI VYAMA HUO NI UNAFIKI WA HALI YAJUU MRADI UMEZALIWA TANZANIA KWENU NI TANZANIA ACHENI KUINGILIA MAMBO YASIO WAHUSU NA WALA MSIJISAHAU

    ReplyDelete
  11. TUNAWAITA "WASAKA TONGE"

    ReplyDelete
  12. wakina nani tena hao wanaoitwa wasaka tonge?

    ReplyDelete
  13. cdm at work.ccm oyeeee

    ReplyDelete
  14. wa bongo bana kwani lazima ucomment kama jambo wewe hutaki si ukae kimya hakuna aliyelazimishwa...katiba ya ccm ndio imeruhusu kuwe na matawi nje ya nchi sasa wanachama wameamua wewe wakerwa na nini?

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake