KAMATI YA AFYA DMV
INATUKUMBUSHIA KUCHUKUWA TAHADHARI KWA MAFUA MAKALI KWA KUPATA CHANJO YA MAFUA SASA
Mafua/influenza (Flu) ni ugojwa wa kuambukiza (contagious disease) ambao husambaa hapa marekani wakati wa masika kati ya mwezi wa 5 na mwezi wa 10 .Mafua haya husababishwa na virusi vilivyo katikavya kundi la Influenza
1. Influenza A (H1N1),
2. Influenza A (H3N2)
3. Influenza B.
Maambukizi ya Ifluenza A & B hupatikana pale unapokuwa karibu na mtu mwenye flu kupitia kukohoa, chafya au kugusana kwa karibu.Yashauriwa kuosha mikono mara kwa mara ili kupunguza maambukizi .Chanjo ya mafua (Flue shot) ni mchanganyiko wa aina tatu za chanjo(Trivalent vaccine) ambazo hukinga watu dhidi ya virusi vya influenza .
DALILI ZA FLU
- Homa ≥ 100F
- Mafua,chafya,kukwaruza kwa koo
- Maumivu ya kichwa,mwili,viungo
- Uchovu wa mwili
- Kichefuchefu,kutapika hata kuharisha
FAIDA YA CHANJO
a) Kukinga mwili na ugonjwa wa mafua makali / influenza (“Flu”)
b) Kupunguza Makali au kukinga kuambukiza mafua kwa watu wengine
NANI ALIYE HATARINI ?
- Watoto (chini ya umri wa miaka mitano)
- Wazee (miaka 65 na Zaidi)
- Wagonjwa wenye kinga hafifu za mwili
- Wanawake Wajawazito
- Wafanyikazi wa vitengo vya afya
- Watu wenye kusumbuliwa na magonjwa ya kisukari, asthma, shinikizo la damu, na sarakani.
CHANJO YA MAFUA BURE AU KWA BEI NAFUU HUPATIKANA HAPA.
Weka appointment kupitia: montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014.
- October 20, 2014 from 4 to 8 pm _Montgomery college: Rockville Campus, 9630 Gudesky Dr, Rockville MD 20850. Giving shots for individuals 6 months of age or older by appointment only. FREE
- October 31, 2014 from 9 am to 12 noon. Kennedy High school, Richard Montgomery high school and Seneca Valley high school for flu mist clinic by appointment only. Schedule appointments on at: Montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014. FREE
- November 3 and 17, 2014 from 1 pm to 4 pm. Silver Spring health center. 8630 Fenton st. Silver Spring, MD 20910: Schedule appointments on at: montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014.FREE
- November 17, 2014 from 8:30 am to 11:30 am – Germantown Health center.12900 Middlebrook Rd, Germantown MD 20874.
- Muslim community clinic (MCC). Clinic ipo New Hampshire ave towards north kwenye majengo ya msikiti.
NOTE: Sehemu ambazo huduma sio bure unaombwa uje na health insurance kadi yako na wale wasio na Health Insurance kutakuwa na chaji ya $20 kulingana na MD kipimo cha umaskini ( MD state poverty sliding scale).
ILI TUSONGE MBELE, AFYA KWA WANADMV KWANZA !
Ref./Thanks
http://www.cdc.gov/flu/about/disease/symptoms
images
1 comment:
Mimi ni mwanajumuiya lakini swala la kamati sina taarifa ziliteuliwa lini? Na je mbona hatujawahi kujulishwa majina ya wanakamati?
Post a Comment