Sunday, October 12, 2014

YUSSUF HAMED BINGWA WA HALUA AFRIKA MASHRIKI

 Bw. Yussuf Hemed akiwa kwenye kazi yake ya kila siku ya kusonga halua.
Akiwa amerithi mikoba ya baba yake Bw.Yussuf Hamed ameendeleza biashara ya halua yenye ubora wa hali ya juu katika duka lake lililopo Wete kisiwani Pemba.Kuanzia asubuhi mapema wateja humiminika kujipatia halua na kahawa na kuendelea na shughuli zao.Hapa Marekani watu hukimbilia Starbucks, basi na huko Wete Pemba hukimbilia kwa Bw.Yussuf Hamed kupata robo kilo ya halua na kahawa na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali.Vile vile oda mbali mbali hupokelewa iwe ni harusi,maulidi au hata hitma katika kuomboleza halua huwa haikosekani.Hivyo siku ukipata bahati ya kutembelea Pemba usikose kupitia kwa Bw.Yussuf upate ladha maridhawa ya Halua ya Lozi ambayo haia mpinzani katika ukanda wa Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake