Saturday, November 1, 2014

YANGA 'YABEBESHWA MKUNGU WA NDIZI' KAITABA BUKOBA

 MASHABIKI WAINGILIA KATI CANAVARO KULIMWA RED, 

MWAMUZI AONDOKA CHINI YA ULINZI

MSHAMBULIAJI Paul Ngway, leo ameiwezesha timu yake ya Kagera Sugar, kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu yaa Tanzania Bara, uliopigwa kwenye Uwanja wa kaitaba mjini Bukoba. Bao hilo pekee lilipatikana katika dakika ya 52.
Yanga SC ilimaliza mchezo huo huku wakiwa pungufu, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 na mwamuzi Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, baada ya kumpiga kichwa Rashid Mandawa wa Kagera.
Ngway, mchezaji mkongwe wa timu hiyo ya Wakata Miwa wa Misenyi, Bukoba Vijijini, alifunga bao zuri kwa shuti kali akimalizia krosi ya Julius Kwangwa.

Yanga SC inabaki na pointi zake 10 baada ya mechi sita, ikishinda tatu, sare moja na kufungwa mbili, nyingine na Mtibwa Sugar mjini Morogoro 2-0.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Yanga SC walimtishia mwamuzi kiasi cha kutolewa uwanjani kwa msaada wa askari wa Polisi.
KAGERA SUGAR; Agathon Anthony, Benjamin Asukile, Abubakar Mtiro, Erick Kyaruzi, George Kavilla, Babu Ally, Julius Ambrose, Paul Maona, Rashid Mandawa, Atupele Green na Adam Kingwande/Paul Ngway dk46.
YANGA SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Nizar Khalfan dk87, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima/Hamisi Kiiza dk72, Genilson Santos ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Jerry Tegete dk54. Sufiani Mafoto

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake