Advertisements

Tuesday, December 23, 2014

Utouh: Dalili za nchi kutotawalika zinaonekana

Aliyekuwa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh amesema mihimili mitatu ya nchi ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali isipofanya kazi bila kuangalia mipaka yao kwa mujibu wa sheria nchi haitatawalika.
Amesema utendaji wa siku kwa siku wa mihimili hiyo unatakiwa kupimwa kwenye mizani ili kila mhimili ufanye kazi bila kuingilia kazi za mihimili mingine kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kulinda amani ya nchi pia kuongeza utawara bora na wenye maadili mema.
Utouh ameyasema haya leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea tuzo ya uadilifu na utawala bora kutoka kwenye kampuni ya Dream  Success Enterprises baada kuutambua umuhimu wa utendaji kazi wake akiwa kazini kabla ya kustaafu.
Amesema ubabe na kutoelewana huku kila mhimili ukitaka kujiona kuwa upo juu ya muhimili mwingine kuna weza kukaleta machafuko makubwa yatakayoigharimu nchi, na kwamba kurudisha amani itachukua muda.
“Kuna haja ya hiii mihimili kufungiwa mizani, kufanya kazi kwa kutoingiliana, pia ikiheshimiana na kutatua mambo yao kwa hekima Tanzania itakuwa sehemu tulivu, yenye amani na kimbilio la wanyonge, lakini kama kila muhimili ukifanya kazi kivyake bila kuzingatia sheria machafuko yanaweza kutokea na kuifanya nchi isitawalike,”anasema Utouh.
Anasema katika harakati zake akiwa kazini atalikumbuka daima sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa katibu Mkuu wa Nishati na Madini David Jairo.
Anasema hayo yote yaliwezekana kufanyika kwa sababu mihimili ya Serikali ilikuwa ikifanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu bila kuingiliana katika maamuzi.
Anasema tuzo aliyopata anaipokea ingawa katika kipindi chake cha kazi ndipo kulipozaliwa jina la ufisadi, hata hivyo amesema anajivunia kuwepo kwake katika ofisi ya CAG kwani alifanikwia kurudisha imani ya chombo hicho kwa wananchi na hivi sasa wananchi wanakiamini
Mwananchi

No comments: