Advertisements

Saturday, January 24, 2015

WANAUME HURU KUJISAIDIA WAKIWA WAMESIMAMA


Mpangaji amekataa kumlipa mmiliki wa nyumba akisema ni haki yake kusimama akiwa anaenda haja ndogo

Mahakama moja nchini Ujerumani imempa idhini mwanamume mmoja kujisaidia haja ndogo akiwa amesimama baada ya mwenye nyumba kutaka alipwe akidai kuwa sakafu ya bafu lake iliharibiwa na mkojo wa mpangaji wake.
Mwenye nyumba ambaye alitaka kulipwa dola 2,200 kwa uharibifu uliofanyika, alidai kwamba sakafu yake iliyotengezwa kwa mawe aina ya Marble iliharibiwa na mkojo.

Lakini jaji aliamua kwamba njia aliyotumia mwanamume huyo kujisaidia inaambatana na tamaduni nyingi akisema kuwa mtu anapojisaidia akiwa amesimama ni jambo la kaiwada sana.

Kuna mjadala nchini Ujerumani kuhusu ikiwa wanaume wanapaswa kujisaidia haja ndogo wakiwa wanasimama au wakiwa wamekaa kwenye choo.

Baadhi ya vyoo nchini Ujerumani haviwaruhusu watu kujisaidia wakiwa wamesimama, lakini wale wanaoamua kuketi chini huitwa "Sitzpinkler", ikimaanisha kwamba wao sio kama wanaume ni sio jambo la kawaida kwa wanaume kukaa wakiwa wanajisaidia haja ndogo.

Jaji Stefan Hank alikubaliana na ripoti ya wataalamu kwamba tindiklia inayotokana na mkojo au Euric Acid, huharibu sakafu nyingi za vyoo.

Lakini kwa kukamilisha amri yake, jaji alisema kwamba wanaume wanaosisitiza kusimama wanapojisaidia haja ndogo, mara kwa mara huvurugana na wenye nyumba lakini hawawezi kuamrishwa kulipa ikiwa sakafu itaharibika.

1 comment:

Anonymous said...

ukikaa na kujisaidia ni bora zaidi kwa mwanamme usisikiye,because mkoja huwa unatoka wote na ukaukamua vizuri,ukisimama na kujisaidia huwa mkojo hamaliziki.labda uchutame kidogo na kuukamua mpaka uishe na una take time.so ni vizuri na ni kiiafya kukaa mwanamme na kujisaidia.

wangaliyeni waislamu ndugu zetu wanavyo fanya ndo inavyotakiwa na sasa mataifa ya kimagharibi yana kopi mambo haya.