Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa ameongozana na watendaji wa Kampuni ya Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa ziara ya kuwabaini wezi wa maji jana. Picha na Kelvin Matandiko, Mwananchi
Makalla amesema udhaifu unaofanywa na watendaji wa Dawasco unasababisha malalamiko mengi kwa wananchi. Alisema hayo jana wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya katika mamlaka hiyo huku akiagiza mameneja hao, Robert Mugabe wa Boko na Peter Chacha wa Kimara Temboni kuondolewa.
Katika maeneo aliyoyatembelea ya Magomeni Kagera, Kimara Temboni na Boko alishuhudia mitandao ya maji ya wizi ikiwa imefungwa maeneo ya wazi na vichochoroni.
“Kinachosikitisha zaidi ni kutokuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi maji yanapokosekana, siwezi kuikubali hali hii. Jana tumekamata wezi 12, nimeagiza wawatafute wengine wakatwe,” alisema Makalla.
No comments:
Post a Comment