Madai hayo ni pamoja na kupewa mikataba bora ya ajira, ambayo itahusisha utaratibu wa ulipwaji wa mishahara ili kuisaidia serikali kukusanya kodi tofauti na ulipwaji wa posho ambao unatumika sasa kupitia huduma za kibenki yazinayotolewa kupitia simu za mikononi.
Wanadai utaratibu huo wa sasa umekuwa ukiwafanya wadhalilike kwa kulipiwa na abiria chakula na kinywaji mahotelini wanapokuwa safarini.
Mengine ni kupinga uamuzi wa serikali wa kuwataka kurudi chuo kusoma wakidai kuwa hakuna jipya wanalokwenda kulisoma.
“Kama madereva kwenda shule kusoma ngazi ya digrii, diploma au cheti tutaenda kama wanavyosoma watu wengine wa kawaida.
Lakini kama ni kwenda kusoma alama za barabarani ambazo kila siku tunacheza nazo barabarani hadi macho hayaoni kamwe hatutarudi shule,” alisema Saleh.
Dai lingine ni kutaka mataa yaliyoko kwenye makutano ya Barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara kuachwa yafanye kazi,badala ya magari kuongozwa na askari wa usalama wa barabarani.
Saleh alisema askari hao wamekuwa wakisababisha msongamano wa magari katika eneo hilo kutokana na kupendelea kwa kuruhusu upande mmoja wa magari yanayotoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuruhusu wageni na pia magari yanayotoka mjini kwenda JNIA.
kupatiwa huduma ya bima ya afya wanapopata ajali, kuingizwa kwenye utaratibu wa kuwekewa akiba kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, kupinga utaratibu wa kuzibana teksi pekee kulipa kodi, huku bajaj zikiachwa kutoa huduma bila kulipa kodi.
Lingine ni utaratibu wa baadhi ya mabasi yanayotoa huduma kati ya Dar es Salaam na nchi jirani kuishia maeneo mbalimbali yaliyoko nje ya UBT, kama vile Kariakoo.
Dai lingine ni kupinga malori kuegeshwa kwa muda mrefu sehemu za mipaka, kama vile Tunduma kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi, ambako alidai wamegundua kuwa katika maeneo hayo kuna baa na nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hivyo kuwachelewesha kwa makusudi ili wapate kufanya biashara.
Lingine ni ukaguzi wa magari kufanyika mara moja kwa wiki ili kuondoa adha za magari kukamatwa mara tatu kwa siku na kuandikiwa malipo ya faini za mara kwa mara, ambao wanadai wakati mwingine ukaguzi huo umekuwa ukifanywa kwa makusudi, hasa katika maeneo ya bandarini.
"Tulitaka waziri mkuu aje atatue mgogoro huu, lakini kumbe kuna ambaye anaweza kuutafutia ufumbuzi, lakini cha msingi sisi si kumtafuta waziri mkuu bali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili, ikizingatiwa kuwa ugomvi wetu siyo sisi na serikali, bali na wamiliki ambao wanatakiwa kutupatia haki zetu za msingi," alisema Saleh.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment