Advertisements

Saturday, May 30, 2015

MH. LOWASSA KUANZA "SAFARI YA MATUMAINI" MCHANA WA LEO

Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

3 comments:

Anonymous said...

This is so badly scripted. Sasa huyo alievaa mkanzu ndo tujue waislamu wamewakilishwa? Why?? This is such a joke and I can't believe Tanzanians are played for fools.

Anonymous said...

This man, Lowassa is a disaster. Wakimpa nchi Tumekwisha.

Anonymous said...

It doesn't matter hata kama aliyevaa kanzu ni muislaam au siyo. Huyo amepigwa picha hata kama amevaa kanzu hilo ni tatizo lake, kwani ninyi waislaam mnayo nini ambayo ni special???