Advertisements

Saturday, June 27, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAKAMU WAKE DKT. BILAL WAWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA GEITA, VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR

 Wapambe wa Bunge wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Max, wakati likiwasili kwenhye Viwanja vya Karimjee.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,  akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni mkewe Mama Salma Kikwete.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max. 
 Sehemu ya waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni...
 Waombolezaji....
 Wanafamilia wakiwa na nyuso za huzuni....
 Waombolezaji.
 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wake, Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

1 comment:

Komango Hill said...

Safari njema Donald Mungu akutangulie