Advertisements

Monday, July 6, 2015

Kauli ya Mbunge Lusinde: Wananchi watoana ngeu.


Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde.Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde, juzi alisababisha mapigano yaliyojeruhi wapigakura wake kadhaa.

Baadhi ya wapigakura wake kumzomea wakipinga hoja zake alizokuwa akitumia kujinadi katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nkwenda wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.
Mkutano uliondaliwa na serikali ya kijiji ili kumpa nafasi mbunge huyo kuzungumza na wananchi wake juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya kwa taktibani miaka minne na nusu.

Alianza kwa kueleza alivyo tumia fedha kutekeleza miradi ya barabara, zahanati, maji pamoja na mambo mengine ambayo yote alisema imegharimu zaidi ya Sh. milioni 400 na vile vile kujinadi kuwa yeye ndiye alileta mradi wa Tasaf na fedha zinazotumika ni za kwake.

Baada ya mbunge kueleza hivyo, kundi la wananchi walianza kuzomea na kupiga kelele kuwa mbunge anadanganya kwa kuwa hakuna miradi ambayo imetekelezwa katika kijiji hicho kwa kiasi cha fedha hizo na za Tasaf ni za serikali sio zake.

“Mbunge huyo ni uongo huwezi kutudunganya hakuna kitu kama hicho baaadhi ya sauti za wananchi zilisikika. Baadhi ya sauti hizo zilisema: ‘

“Mbunge hujafanya kitu, hii miradi sio wewe usindanye wananchi.”

Kutokana kelele hizo zilizodumu kwa zaidi ya dakika kumi na Lusinde kubaini hakuna ayemsikiliza, aliwaeleza wananchi kuwa wakae katika makundi mawili moja wanamuunga mkono na wasio muunga mkono.

“Naomba wale ambao tupo pamoja wakae kulia na wale ambao hatuko pamoja wakae kushoto ili kutambuane kwa vizuri zaidi,” alisema Lusinde.

Baada ya makundi hayo wawili kujitenga huku idadi kubwa ya wanawake ili wale wanaomuunga mkono na wanaume kubaki upande usio muunga mkoano, Lusinde aliwaamuru vijana wapatao 15 kuwashambulia watu wanaopingana naye.

“Sasa nyinyi kama mnajifanya ‘masteling’ basi mimi ni steling zaidi yenu sasa makomando wangu watawashughulikia, sisi tuko tayari hata kufa,” alisema Lusinde.

Baada ya kauli hiyo vijana hao walitoa fimbo na marungu na kuanza kuwashambulia wananchi na kusababisha watu wakaanza kukimbia ovyo na wengine kujificha majumbani kwa kujifungia milango kuhofia kipigo.

Mmoja wa majeruhi hao Yohana Mnyanyi, aliyeshonwa juzi saba, lisema alikuwa akitoka eneo ambalo walikuwa wakichimba kaburi akielekea nyumbani ndipo alipokuna na watu zaidi ya kumi wakiwa wamebeba fimbo na marungu wakikimbiza watu na kuwapiga.

“Mimi wakati nakuja nikakutano na watu wanakimbizana nikauliza kuwa jamii hii ni vita au kitu gani kabla sijamaliza nikapigwa fimbo nikakinga mkononi hapa nilipovimba, lakini pia nikapigwa ya pili kichwani hapa niliposhonwa nyuzi saba na kuaguka chini…lakini mbunge Lusinde naye alikuwepo akisema ngoja leo makomando wangu wafanye kazi yao tuheshimiane,” alisema Mnyanyi.

Saidi Elieza alisema pamoja na watu hao kutumia fimbo lakini pia mmoja wa waopambe wa Mbunge alikuwa ameshikilia panga akisema atayejifanya jeuri atamkata shingo yake.

Alisema kuwa mara baada ya vurugu hizo kuanza walianza kupigwa watu na cha kusikitisha zaidi hadi watu wenye matatizo ya akili walipigwa.

Mganga wa Zahanati ya Kijiji Cha Nkwenda, Elisha Chizuwa, alithibitisha kupokea watu watatu na kuwa wawili kati yao moja alishonwa nyuzi saba, mwingine tano na mwingine alimpatia matibabu ambapo akiwa ameumia ubavuni.
“Nilipatiwa taarifa na ofisa Mtendaji wa Kijiji aliniambia kuwa watu hao wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa mbunge,” alisema.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho Jonas Chitunga, pia alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuiomba serikali kuongeza ulinzi wakati wa mikutano ya kisiasa.

Lusinde alipoulizwa alidai kuwa kuna watu waliokuwa wamenunuliwa pombe za kienyeji ili waharibu mkutano wake na kuwa waliwaomba watulie, lakini walikataa ndipo na wao wakaanza kuwapiga kwa kujihami.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

Anonymous said...

Huyu mbunge Lusinde ni mkosi na hatufai kabisa na wala asijaribu kuomba kura awamu hii..