ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 18, 2015

MADIWANI 17 NA WENYEVITI 39 WA VIJIJI MONDULI WAHAMIA CHADEMA

7 comments:

Unknown said...

Kwa miaka mingi tagu kuanzishwa kwake CCM imejenga misingi ya kutoendekeza au kuupa nafasi upuuzi wa kikabila katika siasa ya nchi yetu na ndio maana tuna nchi hii yetu tamu tunayojivunia leo. Nathubutu kusema hao waliohama C CM huko monduli kwa sababu ya Lowasa wamehama kwa sababu ya ukabila na huko walikokwenda kuhamia wamefuata ukabila bila shaka wataupata huko na wamefika.

Anonymous said...

Kauli yako mtoa maoni hapo juu naifananisha na mtu asiyeelewa mambo. Lowasa siyo hata Mmasai huo ukabila unaozungumzia ni upi. Fanya uchunguzi acha kukurupuka.Watu walikuwa na Imani na Mbunge wao tu na wana uhuru wa kufanya hivyo. Kwani ccm ni kitu gani katika Tanzania yetu. Mwisho wake utafika tu siku moja.

Anonymous said...

Wahame tu kws raha zao bado CCM ni ileile na Watu ni walewale,,, hao timu lowasa wata hangaika sana tu.

Anonymous said...

Nakuunga mkono mdau hapo juu. Tatizo ni kwamba wengi wao bado hawajaelimika...too bad, hii ni 21st century! Sielewi kama Lowasa angewasaidia kwenda shule, kama angepata Urais. Jee, nini aliwatendea alipokuwa Waziri Mkuu, beside competing with fellow Masai men in cattle ownerships?

Anonymous said...

Usiwe mvivu wa kufikiri. Tamko lilisema" Raisi hajayo hatoki kaskazini" Je hao walikuwa wakabila au?

Anonymous said...

Hapana na hasa muasisi wa siasa za Kaskazini? Hili lakusema raisi hawezi kutoka Kaskazini linafumbiwa macho lakini supporters wa mtu fulani wakiamua kubadilisha iti kadi basi tunaita ukanda. What a double standard. Ukabila unaonekana tu upande wa Kaskazini eeh. Huko Simiyu wamehama nao pia sasa huo nao ni ukabila?

Anonymous said...

Mtoa hoja hapo juu unatoa majibu magumu katika swali rahisi, kwa sababu ya kutumia nguvu nyingi kufikiri pasi na sababu. Nina wasi wasi kama mwenendo wako ni huo katika kila nyanja ya kimaisha basi utakuwa na matatizo makubwa. Kwa kifupi watu kama wewe ndio chanzo cha migogoro ya kidini, kikabila, kirangi..nk. Maana mnapenda kulazimishia sababu ngumu ngumu kwenye masuala mepesi. Kumbuka tuhuma za ukabila pamoja na nyinginezo zinazofanana nazo ni hatari kwa mustakabali wa amani. Jibu la hao ndugu kuhama CCM lilitakiwa kuwa jepesi na sio hili lako la kuwabatiza watu UBAGUZI, kumbuka chama sio mama ya mtu, watu wanabadili vyama kuliko nguo, sembuse CCM?